Wachimbaji wadogo wa madini wakiwa eneo karibu na machimbo ya Mwashina wilayani Nzega mkoani Tabora wakikimbia huku na kule baada ya kukutana na polisi |
Ndivyo hali ilivyokuwa |
Pichani ni mmoja kati ya waandamanaji hao aliyekuwa karibu na Dkt Kigwangala akiwa chini baada ya kujeruhiwa na polisi sehemu za usoni |
Mlipuko wa mabomu kwa mbali |
Awali mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kigwangala akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini hao katika kijiji cha Nzega Ndogo kabla ya maandamano |
Maandamano baada ya mkutano wa Dkt Kigwangala kuelekea eneo la machimbo ya Mwashina wilayani NZega. |
Jeshi la polisi
wilayani Nzega mkoani Tabora jana limemkamata
mbunge wa jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya
wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao
ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited.
Kabla ya hapo leo
Machi 24, 2014
mbunge huyo alifanya mkutano mkubwa wa
hadhara na wachimbaji hao katika kijiji cha Nzega Ndogo wilayani humo ambapo
alielezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini
Bw. Paulo masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo kwenye
eneo hilo.
Katika mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vema
serikali iangalie haki zao zilizotumika kwenye uendeshaji na uchimbaji wa
mashimo hayo kuliko kuwafungia bila kujali ingawa eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa
Resolute lakini wao ndiyo wamiliki wa
ardhi hiyo.
Hata hivyo katika hoja hiyo mbunge huyo aliwataka
wachimbaji hao kudai haki yao
kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na
kidini na badala yake wawe kitu kimoja.
Baada ya kauli hiyo mbunge huyo aliwaambia wachimbaji
hao wadogo kuwa haki yao iko mikononi mwao hivyo ni uamuzi wao wa kudai haki
yao na yeye kama mwakilishi wao yuko nyuma yao mpaka pale haki yao
itakapopatikana.
Wachimbaji hao walimwomba mbunge huyo kuambatana nao
kwenye maandamano ya amani kutoka kijiji cha Nzega Ndogo kwenda Mwashina yalipo
machimbo yaliyofukiwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu kujionea hali halisi ya
kufukiwa kwa eneo hilo na ikiwezekana kufanya mkutano mwingine wa hadhara
kijijini hapo.
Kufuata hali hiyo wachimbaji hao walianza maandamano
ambayo yaliungwa mkono na mbunge huyo hadi kijiji cha Mkwajuni kabla ya kufika
Mwashina ambapo polisi waliibuka na kuyasambaratisha maandamano hayo kwa mabomu
ya machozi na risasi za moto.
Katika na
purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu
mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari
pamoja na mbunge huyo.
Awali askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa
habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo
ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda
alipopigiwa simu na waandishi wa habari alisema hana taarifa yoyote kuhusiana
na maandamano hayo, kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Nzega na kutumika kwa
risasi za moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo.
Tayari Dkt Kigwangala ametoka polisi usiku wa kumkia leo
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora