Wachezaji timu ya wanawake Kolandoto wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga-Picha zote na Philipo Chimi-Shinyanga |
Wachezaji timu ya wanawake Shycom
Timu ya Kolandoto kushoto,Shycom kulia
Walimu kutoka Kolandoto wakiwa uwanjani
Mchezo wa netball unaendelea
Shycom wakishangalia
Mpira wa miguu unaendelea
Mchezo unaendelea
Mpira wa kikapu unaendelea
Chuo cha ualimu
mkoani Shinyanga SHY COM jana kiliibuka kidedea katika michezo ya
kirafiki dhidi ya timu kutoka Chuo cha uuguzi Kolandoto mkoani Shinyanga
michezo iliyopigwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.
Katika michezo hiyo ya
kirafiki mchezo wa kwanza ulikuwa ni mpira wa pete (netball)ambapo timu ya chuo
cha ualimu Shinyanga ilitoa dozi ya kuchapa bao 18 kwa sifuri timu ya netball
kutoka Chuo cha uuguzi Kolandoto.
Katika mchezo huo
mchezaji machachari wa timu ya netball Shycom Ratifa Hussein ndiye
alikuwa wa kwanza kufungua pazia hilo la mvua ya magoli kwa tim yake baada ya
kufunga goli safi na hivyo kuonekana kuwa tishio kwa mabeki wa timu ya netball
ya kutoka Kolandoto.
Hadi kipenga cha mwisho
cha mwamuzi kinapulizwa timu ya Shycom magoli 18 Kolandoto 0.
Baada ya mchezo huo
kuisha ulifuatiwa mchezo wa wavu (Volleyball) ambao ulichezwa dakika zote
zikamalizika kwa sare ya timu hizo kufungana seti moja kwa moja.
Kufuatia hali hiyo ilimlazimu
mwamuzi kuongeza muda ili mshindi kupatikana na hatimae tim ya moira wa wavu
kutoka chuo cha uness kolandoto kuibuka na ushindi wa seti mbili kwa moja.
Mchezo uliofuatia
ulikuwa ni mpira wa kikapu ambapo shycom walikubali kupokea kichapo cha
kufungwa vikapu 28 kwa 8 na hivyo kufanya Kolandoto kuibuka na ushindi katika
mchezo huo.
baada ya mchezo
huo ulifuatiwa mchezo wa watu wazima mpira wa miguu ambapo shycom walifanikiwa
kuichapa kolandoto kipigo cha mbwa mwizi kwa kuifunga goli 4 kwa nunge .
Magoli ya Shycom
yaliwekwa kimyani na Ramadhani Songolo dakika ya 10 kipindi cha kwanza ,goli la
pili lilifungwa na Kasungu Kashindye dakika ya 15 kabla ya Bandoma Mtata
kuongeza bao la tatu dakika ya 40 kipindi cha kwanza.
Baada ya mapumziko Ramadhani Songolo kwa mara
nyingine akaongeza msumari wa nne na kuifanya Shycom kuongoza goli 4 kwa 0
,hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Shycom 4 Kolandoto 0.
Baada ya mchezo
kumalizika makaptain wa timu zote mbili Valentina Malima kutoka Shycom na
Jacob Phaustine kutoka Kolandoto walisema mchezo ulikuwa mzuri aliyepoteza
kapoteza kwani mchezo ndivyo ulivyo.
Na Philipo
Chimi-Shinyanga
Social Plugin