Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MTAMBO WA KUCHONGEA BARABARA "GREDA" WAKABIDHIWA MANISPAA YA SHINYANGA



20.03.2015-Hapa ni katika ofisi za manispaa ya Shinyanga ambapo,Kampuni inayojihusisha na uuzaji wa mitambo na magari hapa nchini ya GF Trucks & Equipments Limited ya Jijini Dar es salam leo asubuhi imekabidhi mtambo wa kuchonga wa barabara (Greda aina ya Telex) katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga lililonunuliwa kutokana na fedha kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara-picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog


Greda aina ya Telex likiwa kwenye ofisi za manispaa ya Shinyanga kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa uongozi wa manispaa ya Shinyanga ambapo mstahiki meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alipokea greda hilo lenye thamani ya shilingi milioni 520 ikiwa ni pamoja na gharama za usafirishaji

Chumba cha dereva wa Greda hilo,dereva Mudy akijaribu kuliendesha kabla ya kukabidhi kwa wenyewe

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akingalia matairi na vifaa vingine vya greda hilo

Majaribio yanaendelea-Akikabidhi mtambo huo aina ya Greda kwa meya wa manispaa ya Shinyanga, Gulaam Hafeez Mukadam, Mhandisi wa mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni hiyo Juma Hamsini (kushoto) amesema kampuni yao ilishinda zabuni ya kuuza mitambo kwa manispaa hiyo.

Mstahiki meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam akishuhudia maajabu ya greda hilo

Greda likiwa karibu kabisa na magari mawili yenye thamani ya shilingi milioni 235 yalikabidhiwa na Kampuni inayojihusisha na uuzaji wa mitambo na magari hapa nchini ya GF Trucks & Equipments Limited mapema wiki hii

Hili ndiyo greda lenyewe

Wa tatu kutoka kushoto ni Mhandisi wa mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni hiyo Juma Hamsini akikabidhi ufunguo kwa Mstahiki meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulaam Hafeez Mukadam amesema mtambo uliokabidhiwa utatumika katika ujenzi wa barabara katika manispaa hiyo ambapo watautumia pia kukodi kwa wakandarasi ili kuiongezea mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.
Mhandisi wa mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni inayojihusisha na uuzaji wa mitambo na magari hapa nchini ya GF Trucks & Equipments Limited Juma Hamsini (katikati) amesema mtambo huo wa kuchongea barabara una uwezo wa kutumia lita 1 ya mafuta kwa umbali wa kilomits 3 na ukiweka Full tank unaweza kufanya kazi kwa saa 8 hadi 10 na una uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 20 -picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BOFYA MANENO HAYA KUONA TUKIO JINGINE KUBWA LILILOFANYWA NA KAMPUNI YA GF TRUCKS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com