Tigo Yatangaza Video Za YouTube Kupatikana Bure Usiku



Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mapema jana kuhusu huduma iliyoanzishwa na kampuni hiyo ya kutiririsha video za YouTube bure ambayo itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Kulia ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.



Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.



Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


………………………………………………………………………………………………………..


Dar es Salaam, Aprili 21, 2016 – Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania imetangaza upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za YouTube nyakati za usiku kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa huduma hiyo kwenye mitandao ya kijamii bila tozo hapa nchini.


Akitangaza tukio hilo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia aliviambia vyombo vya habari kuwa huduma ya kutiririsha video za YouTube bure itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.


Ikiwa imezinduliwa Mei 2005, YouTube ni utiririshaji wa video ambao uunatumiwa na wafuasi zaidi ya bilioni 1 duniani kote, takribani theluthi moja yake wakiwa wanatumia intaneti. Huduma hiyo inawapa fursa ya kuangalia video za YouTube kwa muda wa saa nyingi yakiwawo pia mabilioni ya maoni. Aidha inaruhusu mabilioni ya watu kugundua, kuangalia na kushirikiana video ambazo awali zilibuniwa na kubuni jukwaa na kuunganisha, kuhabarisha na kuvutia wengine sehemu mbalimbali duniani.


“Kitu pekee kinachohitajika ili kuweza kupata data za bure katika kutiririsha video za YouTube ni kuwa na aina ya simu itakachoweza data hizo. Tunaamini huduma hii mpya itaendelea kuonesha kujituma kwetu kwenye kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na kuongoza kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubinifu kwa wateja wetu,” alisema Zacharia.



Pamoja na utriririshaji huo watumiaji wa YouTube pia wateja watakuwa na njia mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu ya simu inayojulikana kama YouTube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadaye wakati ambapo muunganisho na itaneti unakuwa haupo au upo chini.


Kwa video ambazo pale ambapo zinapatikana watumiaji wanaweza kuchagua kuongeza video kwa kuzitiririsha na kwa ajili ya kuangalia hapo baadaye kwa kutumia kitufe cha ‘offline’. Ikiwa imeshachukuliwa kwa njia hiyo video hiyo inaweza kuchezeshwa bila kuunganishwa na intaneti kwa muda wa hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za YouTube bila hofu ya maunganisho na intaneti kuwa yapo chini.


Zacharia aliongeza kwamba kuzifikia data bure kutakuwa kunapatikana kwa wateja wa Tigo wa huduma ya malipo kabla bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika kuifurahia huduma hiyo. Upatikanaji bure wa data za huduma ya kutiririsha video za YouTube umefanyika baada ya kampuni hiyo ya simu kutangaza huduma nyingine ya bure ya WhatsApps kwa wateja wake mwanzoni mwa mwaka huu ambako pia kulitamnguliwa na kiuzinduliwa kwa huduma ya Facebook ya Kiswahili mwaka 2014.


Tigo inayofuraha kujumuisha majkuwaa ya video kwenye ofa hii. Kama wewe ni msambazaji wa huduma ya video unaweza kuwasiliana nasi kupitia customercare@tigo.co.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527