Leo Jumamosi,Agosti 27,2016 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendelea kufanya mazoezi ya utayari wa kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
Akiongoza mazoezi hayo,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema mazoezi hayo aliyoyataja kwa jina la Kiingereza ““Route Match” ni ya kawaida kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana na uhalifu unaoweza kujitokeza.
Kamanda Muliro amesema wamekuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara lakini kilichofanyika leo ni kubadilisha muda wa kufanya mazoezi na wataendelea kufanya kila siku za Jumamosi.
“Huu ni mfumo wa kawaida kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazolisimamia jeshi la polisi..tumefanya matembezi yanayohusiana na ukakamavu, yanayojenga ujasiri kwa askari kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake,kwa wananchi wanaoishi karibu na kambi ya jeshi siyo wageni wa mambo haya ambayo huwa tunayafanya mara kwa mara”,alieleza Muliro.
“Kilichofanyika leo tumepita katika maeneo mbalimbali kuanzia asubuhi saa tatu hadi mchana badala ya usiku/alfajiri (saa 11 hadi saa 1.30)",alisema.
"Niwaondoe tu hofu wananchi kuwa mazoezi haya hayana uhusiano wowote na operesheni UKUTA...naomba wananchi pia watambue tu kuwa jeshi lao la polisi liko imara katika kuwalinda raia na mali zao,kusimamia sheria za nchi na askari mzuri ni yule mkakamavu,mwepesi ana uwezo wa kufikiri haraka kujua kile anachokitekeleza kimesimamia sheria gani”,aliongeza Muliro.
"Niwaondoe tu hofu wananchi kuwa mazoezi haya hayana uhusiano wowote na operesheni UKUTA...naomba wananchi pia watambue tu kuwa jeshi lao la polisi liko imara katika kuwalinda raia na mali zao,kusimamia sheria za nchi na askari mzuri ni yule mkakamavu,mwepesi ana uwezo wa kufikiri haraka kujua kile anachokitekeleza kimesimamia sheria gani”,aliongeza Muliro.
Alisema mazoezi hayo ni ya kawaida na kusisitiza kuwa kwa wananchi ambao siyo wahalifu na walio wema wamefurahia mazoezi hayo.
Askari polisi wakiongozwa na kamanda Muliro walipita katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga na maeneo huku wakiwa na vifaa mbalimbali vya jeshi hilo ikiwemo magari,silaha na magari ya maji ya kuwasha.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo maeneo mbalimbali walikopita askari polisi mjini Shinyanga,ametuletea picha 30…Shuhudia hapa chini
Hapa ni katika kambi ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga -Kulia ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa maelekezo kwa askari wa jeshi hilo kabla ya kuanza mazoezi mitaani leo majira ya saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akieleza kuhusu mazoezi ya "Route Match"
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo kabla ya kuanza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini kabla ya kuanza kufanya mazoezi mtaani
Askari polisi wakijiandaa kuanza kufanya mazoezi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifanya mazoezi na askari polisi wa jeshi hilo mjini Shinyanga
Askari polisi wakiendelea na mazoezi mtaani
Askari polisi wakiwa katika gari la maji ya kuwasha
Mazoezi yanaendelea katika eneo la Phatom mjini Shinyanga
Gari la maji ya kuwasha likiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Mazoezi yanaendelea
Askari polisi wakiwa ndani ya gari
Wananchi wakiendelea na shughuli zao huku askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Wananchi wakiendelea na safari zao
Askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi mtaani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza kambini ambapo aliwaambia askari polisi kuwa watakuwa wanafanya mazoezi ya namna hiyo kila siku za Jumamosi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini
Askari polisi wakimsikiliza kamanda Muliro
Kamanda Muliro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Waandishi wa habari wakiwa kambini
Mmoja wa maaskari polisi waliofanya mazoezi leo Rhobi Wambura akielezea kuhusu mazoezi mbalimbali wanayofanya kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana na uhalifu.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog