Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Askari Polisi Wanne Wauawa Jijini Dar es salaam


Habari zilizotawala katika mitandao ya kijamii usiku wa Agosti 23, 2016 ni kuhusu kuuawa kwa askari polisi wanne kufuatia tukio la uporaji lililotokea katika bank ya CRDB tawi la Mbande, Mbagala jijini Dar es salaam.


Wanaodaiwa kufariki dunia ni E5761 CPL YAHAYA,F4660 CPL HATIBU na G9544 PC TTITO,jina la askari mwingine bado hatujalipata.

Inasemekana majambazi wameondoka na SMG moja.

Inadaiwa kuwa tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo na kwamba mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.

Taarifa zinasema kuwa majambazi hayakuingia ndani ya bank.

Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio

Waziri Nchemba amesema…>>>"Kumetokea shambulio la uvamizi lenye nia ya uovu ambalo limeua askari wanne, vijana wamefika na wataendelea na msako kuhakikisha waharifu wote wametiwa nguvuni"

Bofya HAPA kuona Picha za Tukio hili   
 "Tukio lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ambapo bado uchunguzi unaendelea na taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi, kifupi ni kwamba shambulio lilifanywa kwa kutumia usafiri wa pikipiki na niwakati vijana wakibadilishana lindo lakini niwahakikishie wananchi kuwa watuhumiwa wote watatiwa hatiani" –Waziri Mwigulu Nchemba

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hili>> "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi"

BOFYA HAPA..KUONA PICHA NA HABARI KAMILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com