Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha!! VIFAA VYA KUANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) VILIVYOIBIWA KISHAPU-SHINYANGA VIMEPATIKANA...VIMEKUTWA NYUMBANI KWA MLINZI WA HALMASHAURI

Oktoba 12,2016 saa mbili na nusu asubuhi-Hapa ni katika ukumbi wa mikutano ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga .Pichani katikati ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akionesha kamera za NIDA kwa waandishi wa habari, zilizokuwa zimebiwa zilizokuwa zinatumika kama sehemu ya kuchukua kumbukumbu za watumishi wa umma.Kamera hizo zilikuwa katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Kamanda Muliro akionesha kamera zilizokuwa zimeibiwa

Kamanda Muliro akionesha kamera hizo

Kamanda Muliro akionesha stand za kamera zilizokuwa zimeibiwa

Waandishi wa habari wakichukua matukio

*****

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kuvipata vifaa vya Uandikishaji wa Vitambulisho vya taifa (NIDA) vilivyoibiwa katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.Anaripoti Mwandishi wetu Kadama Malunde.

Vifaa hivyo  ambavyo ni kamera mbili aina ya Canon zenye namba TZNID 01546 na TZNID 01559 na viegesha vyake viwili (Stand) vyenye thamani ya shilingi 6000,000/= viliibiwa Oktoba 10,2016 katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu ghorofa ya kwanza chumba namba 46.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema vifaa hivyo vimepatikana Oktoba 11,2016 saa nne na nusu asubuhi nyumbani kwa mlinzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kufuatia operesheni iliyohusisha makachero wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi.

Alisema baada ya kufanya msako mkali wa kuwakamata watumishi wa halmashauri hiyo na kuwahoji kwa kina,walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wakiwemo walinzi watatu na mhudumu wa masjala ya wazi katika halmashauri ya wilaya hiyo ambao walikiri kuiba kamera hizo zilizokuwa zikitumika kama sehemu ya kuchukua kumbukumbu za watumishi wa umma.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni James Edward(38) mhudumu wa masjala ya wazi katika halmashauri ya Kishapu pamoja na  walinzi watatu ambao ni Mustapha Mabula(24),Cosmas Joseph (22),Silvanus Shija( 47) wote walinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suprem International Limited inayolinda jengo la halmashauri hiyo wote wakazi wa Mhunze wilayani humo.

Alieleza kuwa vifaa hivyo vinavyotumika katika zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma vilikutwa nyumbani kwa mlinzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mustapha Mabula(24) mkazi wa Mhunze wilayani humo.

“Baada ya kuwafanyia mahojiano walikiri kuiba kamera mbili na viegesha vyake viwili mali ya NIDA na kwamba mbinu iliyotumika kutenda kosa hilo ni kutumia funguo bandia ambao huzitumia kuingia kwenye ofisi mbalimbali na kuiba mali”,alieleza Kamanda Muliro.

Aliongeza kuwa pamoja na kukuta mali za NIDA nyumbani kwa mlinzi huyo Mustapha Mabula pia walifanikiwa kupata vitu vingine vilivyoibiwa ndani na nje ya wilaya ya Kishapu.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni magodoro matatu ya hospitali,Kompyuta moja,External hard disk GB 500,Star light mbili,key board moja,CPU moja,Sub wofer moja,Stablizer moja,Wireless Decorder moja,Marker pen boksi moja,kalamu boksi tatu,note book dazani moja,themometa moja,ubao wa meza ya ofisi na kioo kimoja cha kabati la ofisi.
yo vimepatikana.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni Sita vimekutwa vimehifadhiwa chini ya ardhi nyumbani kwa mmoja wa walinzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi limefanikiwa kupata kamera mbili zilizokuwa zimepotea katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

“Oktoba 10,2016 saa mbili asubuhi kulikuwa na taarifa za kupotea kwa kamera mbili na viegesha vyake ikiwa ni sehemu ya vifaa vinavyotumika kama sehemu ya kuchukua kumbukumbu za watumishi wa umma…..Oktoba 11,majira ya saa nne na nusu asubuhi tulifanikiwa kuvipata vifaa hivyo vikiwa nyumbani kwa mlinzi wa halmashauri hiyo Mustapha Mabula (24)”,ameeleza Kamanda Muliro.

“Tumefanikisha kukamata vifaa hivi vikiwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wanne vikiwa vimefukiwa chini ya ardhi..hii inatokana na jeshi la polisi kuendesha zoezi la kukamata watu mbalimbali wakiwemo walinzi na wafanyakazi wa halmashauri ya Kishapu,tumekamata watuhumiwa wanne halisi wakiwemo mfanyakazi wa masjala ya wazi na walinzi watatu”,ameongeza Kamanda Muliro.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni James Edward(38) mhudumu wa masjala ya wazi katika halmashauri ya Kishapu pamoja na walinzi watatu ambao ni Mustapha Mabula(24),Cosmas Joseph (22),Silvanus Shija( 47) wote walinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suprem International Limited inayolinda jengo la halmashauri hiyo wote wakazi wa Mhunze wilayani humo.

Hata hivyo pamoja na kukuta mali za NIDA nyumbani kwa mlinzi huyo Mustapha Mabula pia walifanikiwa kupata vitu vingine vilivyoibiwa ndani na nje ya wilaya ya Kishapu.

Amevitaja vitu hivyo kuwa ni magodoro matatu ya hospitali,Kompyuta moja,External hard disk GB 500,Star light mbili,key board moja,CPU moja,Sub wofer moja,Stablizer moja,Wireless Decorder moja,Marker pen boksi moja,kalamu boksi tatu,note book dazani moja,themometa moja,ubao wa meza ya ofisi na kioo kimoja cha kabati la ofisi.

Amesema watuhumiwa wote wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi na watafikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika. 


Na Kadama Malunde- Malunde1 blog

BOFYA <<HAPA>> KUSOMA HABARI KUHUSU VIFAA KUIBIWA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 11,2016 katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab TelackWaandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga

-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com