Hapa ni katika viwanja vya Zimamoto Nguzo Nane mjini Shinyanga ambapo leo Ijumaa Desemba 02,2016 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekutana wakazi wa Shinyanga katika mkutano wa kusikiliza kero ardhi za wananchi.
Katika mkutano huo uliodumu kwa takribani saa nne waziri Lukuvi amepokea kero zaidi ya 200 za ardhi mkoani Shinyanga zinazodaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na maafisa ardhi,wenyeviti wa mitaa waliojikuta wakishindwa kujibu kero hizo mbele ya waziri huyo.
Waziri Lukuvi alisema baada ya kupokea kero hizo ataunda kikosi maalum cha wataalam watakaoweka kambi mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na wataitwa mmoja mmoja kisha kujibiwa kwa maandishi.
“Kama mmekaa na kero za ardhi tangu mwaka 2008 mpaka leo,naomba mniamini basi mimi kwa sababu waziri ndiyo mwenye majibu ya mwisho kuhusu kero zenu,nilichobaini viongozi hawasikilizi kero za wananchi, kuna kero zingine hazikupaswa kuletwa kwangu mngemalizana huko huko”,alieleza waziri huyo.
“Kama kuna maafisa ardhi wamekuwa sehemu ya migogoro ya ardhi lazima wawajibishwe,haiwezekani wananchi waichukie serikali kwa sababu ya watendaji wasio waaminifu,kiongozi atayebainika kuigombanisha serikali na wananchi tutaachana naye”,aliongeza Lukuvi.
Waziri Lukuvi ametoa wito kwa wananchi wenye kero za ardhi wanapotoa ushahidi wawataje kwa majina watu wote waliohusika katika kukuza migogoro ya ardhi na kusababisha wananchi kunung’unika kwa kukosa haki zao ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kufuatia udhaifu huo aliwataka viongozi akiwemo mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kupanga muda wa kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza kero za wananchi.
Wakizungumza mbele ya waziri huyo,wananchi walisema baadhi ya watendaji wa serikali,wenyeviti wa mitaa na maafisa ardhi wamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro kwa kuendekeza rushwa na kujuana.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika mkutano huo,ametusogezea picha 25 ..angalia hapa chini
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akisikiliza kero za wananchi katika viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga.Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema),akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Mkazi wa Shinyanga mjini akielezea kero ya ardhi huku akiwatuhumu maafisa ardhi kuwa wanaendekeza rushwa na dhuluma kwa wananchi
Mkazi wa Shinyanga akikabidhi nyaraka za mgogoro wa ardhi kwa waziri Lukuvi
Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono kueleza kero zao kwa waziri Lukuvi
Kushoto ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwadui katika manispaa ya Shinyanga Kisena Masengwa akieleza kero za wananchi kwa waziri
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema) akiangalia nyaraka za migogoro ya ardhi ya wananchi wa kata yake
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia nyaraka za kero ya ardhi kutoka kwa mkazi wa Shinyanga aliyedai kukosa haki yake
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia nyaraka za malipo ya mkazi wa Shinyanga
Mwananchi akieleza kero ya ardhi mbele ya waziri
Mkutano unaendelea
Mkazi wa Shinyanga Neema Sonda akikabidhi nyaraka za mgogoro wa ardhi anaokabiliana nao
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kero za ardhi
Kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akijieleza mbele ya waziri Lukuvi
Mwananchi akieleza kero yake kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Wananchi wakiwa katika foleni kukabidhi bahasha za kero za ardhi
Wananchi wakiendelea kupeleka kero zao kwa waziri
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitatua mgogoro wa ardhi kwa wananchi wawili waliodhurumiana nyumba
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitatua mgogoro wa nyumba katika mkutano huo
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza baada kupokea kero zaidi ya 200 za ardhi ambapo alitoa agizo kwa wakazi wa Shinyanga wanaomiliki nyumba kulipia hati hadi ifikapo tarehe 30,Machi 2017 baada ya kubaini kuwa nyumba 16,800 hazina hati huku akisisitiza wananchi kulipia na kutunza hati hizo.
Waziri Lukuvi alitoa wito kwa wananchi wenye kero za ardhi wanapotoa ushahidi wawataje kwa majina watu wote waliohusika katika kukuza migogoro ya ardhi na kusababisha wananchi kunung’unika kwa kukosa haki zao ili waweze kuchukuliwa hatua.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka maafisa ardhi kufika kwa wananchi na kuwapimia ardhi wananchi huku akiwataka wananchi kujitokeza kupata hati zao
Telack aliwataka wananchi kutunza hati zao kwani ndiyo silaha yao pale panapotokea mgogoro wa ardhi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Angalia <<HAPA>>Picha 30: WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AKISIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYANI KISHAPU
Angalia <<HAPA>>Picha 30: WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AKISIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYANI KISHAPU
Social Plugin