Gari la msanii Darassa likiwa limeharibika baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga leo Jumapili Desemba 18,2016
Gari la msanii Darassa likiwa limeharibika baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga leo Jumapili Desemba 18,2016
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA
AJALI YA GARI KUACHA NJIA , KUPINDUKA , KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA GARI. TAREHE 18/12/016 SAA 15:00,HUKO KATIKA KIJIJI CHA NTOBO , KATA YA NTOBO ,TARAFA YA MSALALA ,(W) YA KAHAMA MKOA WA SHINYANGA ,GARI REG NO T 503 DGQ TOYOTA DARK BLUE HARRIER MALI YA SHARIF S/O THABIT RAMADHAN @DARASSA BOX DSM ,MNYAMWEZI ,MIAKA 28 , IKIENDESHWA NA YEYE MWENYEWE ILIACHA NJIA ,KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERAHA KWA SWITBERT S/O CHARLES ,MSUKUMA ,MIAKA 24 ,PRODUCER WA MUZIKI ,MKAZI WA DSM AMBAYE AMEPATA MICHUBUKO MIKONO YOTE MIWILI ,PIA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA GARI HILO.
MAJERUHI AMETIBIWA KITUO CHA AFYA CHA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI .
CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDOKASI WA DEREVA WA GARI HILO.
HATUA ZINGINE ZA KISHERIA ZOTAFUATA.
IMETOLEWA NA MULIRO JUMANNE MULIRO -RPC SHINYANGA.
TAZAMA VIDEO HAPA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA
Social Plugin