Serikali imewaondoa hofu wananchi wilayani Shinyanga kuwa hakuna atakaye kufa kwa njaa kwani kuna chakula cha kutosha kwenye ghala la kuhifadhi chakula.
Akizungumza leo wakati alipotembelea ghala la chakula la Mjini Shinyanga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama, amesema ghala hilo lina tani 6050 na kilo 969 za mahindi na kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wananchi baada ya kuibuka watu wanaopotosha kuwa serikali haina chakula kwenye maghala yake.
Naye wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Shinyanga Mary Shangali amesema mpaka sasa kanda ya Shinyanga inayounda mikoa minane inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara,Tabora,Kigoma,Geita,Kagera na Shinyanga ina jumla ya tani 9146.916.
Amesema pia wanatarajia kupokea chakula kingine kutoka Mpanda mkoani Katavi tani 10,000 na hivyo kanda itakuwa na jumla ya tani zaidi ya 19,000 pindi zitakapofika.
SOMA HABARI KAMILI >>HAPA<<
SOMA HABARI KAMILI >>HAPA<<
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(aliyevaa nguo nyekundu) akiangalia chakula katika ghala la chakula mjini Shinyanga alipotembelea ili kujionea hali halisi ya chakula katika ghala hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(aliyevaa nguo nyekundu) akiangalia mahindi katika ghala la chakula mjini Shinyanga
Kulia ni wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Shinyanga Mary Shangali akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya Josephine na kumweleza kuwa chakula kipo cha kutosha tena kina ubora
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(aliyevaa nguo nyekundu) akizungumza katika ghala la chakula ambapo aliwataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaosema maghala ya chakula hayana chakula
Ndani ya ghala la chakula wilaya ya Shinyanga
Chakula kikiwa kwenye ghala
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Social Plugin