Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga limemsimika katika utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel katika kanisa la AICT Bushushu lililopo kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga.
Ibada maalumu ya kumsimika katika utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel imefanyika jana Jumapili Februari 12,2017 katika kanisa ambalo anakwenda kulitumikia la AICT Bushushu.
Mgeni rasmi katika ibada hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano,alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Mwinjilisti Esther Emmanuel aliyetokea katika kanisa la AICT Kambarage anachukua nafasi ya aliyekuwa mwinjilisti wa kanisa la AICT Bushushu Julius Kamata ambaye ni mtumishi wa serikali.
Mwinjilisti Esther Emmanuel ana uelewa mpana katika mambo ya uinjilisti na amepokea mafunzo mbalimbali ya uinjilisti nchini Kenya,pia amepata mafunzo ya sinema.
Mbali na kubobea katika mambo ya unjilisti,mwinjilisti Esther Emmanuel amepata mafunzo ya kutosha kuhusu huduma za jamii ikiwemo ya ndoa na mahusiano pamoja na watoto.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa Ibada ya Kusimikwa katika Utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel katika kanisa la AICT Bushushu,ametuletea picha 38 za matukio katika picha..Tazama hapa chini
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akitoa neno wakati wa ibada hiyo
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano,akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro aliyekuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo
Wazee wa kanisa la AICT Kambarage ambako ndiko ametokea mwinjilisti Esther Emmanuel wakiwa katika ibada
Viongozi mbalimbali wa dini kanisa la AICT na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro wakisoma vitabu vya mungu wakati wa ibada hiyo
Katikati ni Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akiomba wakati wa Ibada maalumu ya kumsimika katika utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel,kushoto ni Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano,kulia ni Mchungaji David Kazimoto kutoka kanisa la AICT Pastoreti ya Kitangiri.
Wa pili kushoto ni Mchungaji David Kazimoto kutoka kanisa la AICT Pastoreti ya Kitangiri akiomba wakati wa ibada hiyo
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano akiongoza ibada maalumu ya kumsimika katika utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel katika kanisa la AICT Bushushu ambapo alimuomba mtumishi huyo kusimama imara na kudumu katika maombi na kuwataka waumini wa kanisa hilo kumpa ushirikiano mwinjilisti Esther Emmanuel.
Tunafuatilia kinachoendelea hapa
Waumini wakiwa eneo la tukio
Waumini wakifuatilia ibada
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano akiwahasisha waumini kushirikiana na mtumishi wa mungu Esther Emmanuel
Washiriki wa ibada hiyo wakiwa wamenyoosha mikono wakati wa ibada hiyo
Kwaya ya AICT Bushushu wakiimba
Kwaya ya Wazee ikiimba wakati wa Ibada maalumu ya kumsimika katika utumishi Mwinjilisti Esther Emmanuel
Waimbaji wa kwaya ya Akina Mama kutoka kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga wakicheza na kuimba
Akina Mama wakiendelea kuimba
Waumini wa kanisa la AICT Bushushu na wageni waalikwa katika ibada hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Katibu Msaidizi Kanisa kuu la AICT Kambarage Onesmo Maligisa James akizungumzia sifa za Mwinjilisti Esther Emmanuel ambapo alisema amebobea katika mambo ya injili na masuala ya kijamii
Wainjilisti wakitoa neno la kumwongoza mwinjilisti mwenzao Esther Emmanuel (aliyekaa kulia)
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akimsimika katika Utumishi mwinjilisti Esther Emmanuel ili atumikie kanisa la AICT Bushushu
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta ,Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mchungaji David Kazimoto kutoka kanisa la AICT Pastoreti ya Kitangiri wakimuombea mwinjilisti Esther Emmanuel
Wachungaji wakiendelea na maombi
Wachungaji wakimpongeza Mwinjilisti Esther Emmanuel
Mchungaji David Kazimoto kutoka kanisa la AICT Pastoreti ya Kitangiri akishikana mkono na mwinjilisti Esther Emmanuel
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro aliyekuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa ibada hiyo ambapo alimshukuru mwenyezi mungu kwa kumwinua mwinjilisti Esther Emmanuel akidai kuwa anamfahamu kuwa ni mtumishi mzuri
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kufikisha neno la mungu katika maeneo ya vijijini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiendelea kuzungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimpongeza kwa kumkumbatia mwinjilisti Esther Emmanuel
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimpongeza mwinjilisti Esther Emmanuel
Mwinjilisti Esther Emmanuel akicheza wakati kwaya ya Akina Mama kutoka kanisa la AICT Kambarage ikihubiri kwa njia ya wimbo
Akina mama wakiendelea kumpongeza mwinjilisti Esther Emmanuel
Bibi akionesha furaha yake
Mwinjilisti Esther Emmanuel akiendelea kucheza
Mwinjilisti Esther Emmanuel akitoa neno la shukrani baada ya kusimikwa katika utumishi ambapo alimshuru mungu kwa hatua hiyo na kudai kuwa amevumilia kwa muda mrefu kwani wainjilisti wenzake aliosoma nao nchini Kenya tayari wana makanisa yao
Mwinjilisti Esther Emmanuel akiomba ushirikiano kutoka kwa waumini wa kanisa la AICT Bushushu
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Jacob Mapambano akiongozana na mgeni rasmi Mheshimiwa Josephine Matiro kuingia katika kanisa na AICT Bushushu lililopo katika kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga
Picha ya pamoja na mgeni rasmi
Mgeni rasmi mheshimiwa Josephine Matiro akiwa na viongozi wa dini.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin