Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO DENMARK YATOA MSAADA WA NGUO KITUO CHA WAZEE KOLANDOTO NA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA


Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark imetoa msaada wa nguo kwenya kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Kolandoto na kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo wa nguo,Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba alisema ni jambo jema kusaidia watu wenye mahitaji kutokana na kile kidogo walichojaliwa.

“Tunatambua kuwa wapo watu wenye mahitaji muhimu,ndiyo maana tumefika hapa kuwapa hiki kidogo hawa watoto wetu wenye ualbino na wazee wasiojiweza”,alieleza Tumba.

“Lakini kupitia msaada huu tunapenda kuwakumbusha watanzania wengine walio nje ya nchi kwamba wasiwasahau katika nchi yao kwamba kuna watanzania wanahitaji msaada,lakini pia kuikumbusha jamii kuwa wapo watanzania walio nje ya nchi wanaowakumbuka watanzania wenzao”,aliongeza Tumba.

Zawadi hiyo ya nguo imetolewa siku mbili tu baada ya Jumuiya hiyo ya Watanzania waishio Denmark kutoa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.Soma zaidi <<HAPA>>

Vifaa tiba vimeletwa mkoani Shinyanga kutokana na Ushirikiano mkubwa uliofanywa na Diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema) na shirika la AGAPE la mjini Shinyanga ambao walifanya mawasiliano na jumuiya hiyo kuwaeleza jinsi gani wananchi wa Shinyanga wanahitaji msaada kutoka jumuiya hiyo.

Vifaa tiba hiyo tayari vimeshaanza kusambazwa kwenye vituo husika lakini pia kugawa baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo..Tazama <<HAPA>>

Tumba yupo mkoani Shinyanga kufuatilia kama kweli vifaa tiba walivyotoa vinawafikia walengwa.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akikabidhi zawadi ya nguo kwenye kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto na watoto wenye ualbino cha Buhangija,Tazama picha hapa chini
Hapa ni katika kituo cha kulelea wazee waliojiweza cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.Aliyesimama ni  Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la mjini Shinyanga John Myola akimtambulisha Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba na Diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema).Kulia ni Msimamizi wa kituo hicho Sophia Kang'ombe.Kushoto ni mwenyekiti wa kituo hicho cha Kolandoto Mzee Samora Maganga
Msimamizi wakituo cha kulelea wazee waliojiweza cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ,Sophia Kang'ombe akizungumza wakati wa kupokea msaada wa nguo zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark kwa ajili ya wazee waishio katika kituo hicho ambapo sasa wapo 12 na vijana wawili.
Aliyesimama ni Diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (Chadema) akielezea namna ambavyo jumuiya hiyo imeweza kufika katika manispaa hiyo kutokana na jitihada zake na shirika la AGAPE na kufanikiwa kuleta vifaa tiba kwa ajili ya hospitali na zahanati lakini pia kutoa msaada wa nguo katika kituo hicho
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akizungumza katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Buhangija ambapo alisema watanzania waishio Denmark wametoa msaada wa nguo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya wazee hao
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akimvalisha koti mwenyekiti wa kituo cha wazee cha Kolandoto,Mzee Samora Maganga
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimfunika blanketi mzee Samora Maganga
Mzee Samora Maganga akiwa amevaa koti na kufunikwa blanketi
Diwani Emmanuel Ntobi akimsaidia mzee Samora Maganga kuweka sawa koti lake,kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la mjini Shinyanga John Myola akiwa ameshikilia nguo zingine
Mzee Samora akitabasamu baada ya kuvaa koti
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba na Diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi wakimvalisha blanketi mmoja wa wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akiendelea kuwavalisha nguo na kuwafunika mablanketi wazee hao
Mzee Samora Maganga akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa nguo ambapo aliwataka watanzania walioko ndani na nje ya Tanzania kuwakumbuka wazee hao huku akitaja baadhi ya changamoto katika kituo hicho kuwa ni uhaba wa chakula na umeme
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akiwaaga wazee hao huku furaha ikiendelea kutawala kituoni hapo
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino,wasioona na wasiosikia cha Buhangija kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi  akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa nguo zilizotolewa na Jumuiya ya watanzania waishio nchini Denmark
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa nguo kwa ajili ya watoto wenye ualbino cha Buhangija ambapo alisema watanzania waishio Denmark wanawapenda sana watoto hao ndiyo maana wamejitokeza kutoa msaada huo wa nguo
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akifurahia jambo na watoto hao
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akijiandaa kumvalisha nguo mtoto mwenye ualbino katika kituo cha Buhangija
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba  akimvalisha nguo mtoto
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akimkabidhi nguo mtoto mwenye ualbino
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akiendelea kuwapa nguo watoto hao
Kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba akiongea na mtoto baada ya kumkabidhi nguo,Kulia ni diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akifurahia jambo na mtoto mwenye ualbino baada ya kumfunika blanketi
Wa kwanza kulia ni Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimkabidhi nguo Mwalimu Mlezi wa kituo cha Buhangija Anna Onesmo (katikati) kwa ajili ya kugawa nguo hizo kwa watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo hicho

Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE John Myola,Mwalimu mlezi Anna Onesmo,Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Denmark Tambwe Tumba ,watoto na diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi wakifurahia wakati wa makabidhiano hayo ya nguo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com