Jumla ya watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita wamekutana jijini Mwanza katika kambi ya Ariel ‘Ariel Camp’ iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Tanga,Geita na Mara.
Watoto na vijana hao wanaotoka katika vituo mbalimbali vya afya katika mikoa husika, wameweka kambi ya siku tano jijini Mwanza ambapo wanajifunza mambo mbalimbali ya afya kama vile afya ya ujana na makuzi, lishe, stadi za maisha, elimu sahihi kuhusu VVU na Ukimwi, ufuasi mzuri wa dawa,unyanyapaa na ubaguzi na kushiriki katika michezo sambamba na kubadilishana mawazo.
Akizungumza wakati kufungua kambi hiyo,leo June 20,2017, Mkurugenzi wa Miradi kutoka AGPAHI,Dk. Safila Telatela alisema kupitia kambi za Ariel watoto na vijana hupata ushauri wa kisaikolojia kutokana na changamoto wanazokutana nazo na huduma za kitabibu kutoka kwa madaktari wa watoto.
“Mbali na kuwapatia elimu pia tumepanga kuwapeleka washiriki kutembelea makumbusho ya kabila la Kisukuma-Bujora ili kujifunza tamaduni na mila za Kisukuma”,alisema Dk. Telatela.
“Hii ni kambi ya nane tangu kuanzishwa kwa shirika hili mwaka 2011,utaratibu huu wa kuwapeleka watoto na vijana kwenye kambi zilizopo maeneo tofauti ni mzuri kwani unasaidia kuwafundisha mambo mengi kuhusu nchi, historia na tamaduni bila kusahau masomo wanayopata wakiwa kambini”,aliongeza Dk.Telatela.
Katika hatua nyingine alisema AGPAHI imeongeza wigo wa kazi zake kutoka mikoa miwili ya awali ya Shinyanga na Simiyu hadi sita kwa kuongeza mikoa minne ya Mwanza,Tanga,Geita na Mara ikishirikiana na halmashauri za wilaya pamoja na hospitali,zahanati na vituo vya afya vya serikali na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini.
Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo,alikuwa Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Maselle ambaye alilipongeza shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kuwakutanisha watoto na vijana na kuwafanya kuwa mabalozi wa huduma za watoto katika jamii.
AGPAHI ni asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2011 kwa lengo la kutokomeza Ukimwi kwa watoto nchini Tanzania.
AGPAHI inatekeleza majukumu yake kwa hisani ya Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique).
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KAMBI YA ARIEL SIKU YA KWANZA NA YA PILI
SIKU YA PILI:Mgeni rasmi/Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Maselle akizungumza wakati wa kufungua Kambi ya Ariel katika hoteli ya Lesa Garden jijini Mwanza.
SIKU YA PILI:Mgeni rasmi/Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Maselle akizungumza wakati wa kufungua Kambi ya Ariel katika hoteli ya Lesa Garden jijini Mwanza.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela na Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
Dk. Maselle akizungumza na washiriki wa kambi ya Ariel.Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akifuatiwa na Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita Dk. Joseph Odero. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la AGPAHI, Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufungua kambi hiyo.
Dk.Telatela aliwasihi watoto na vijana kuzingatia elimu na kanuni za afya kama wanavyoelekezwa na wataalam wa afya na waendelee kuwa wanachama wazuri katika vikundi vyao 'Ariel Clubs' na wawe mabalozi wa kuwahamasisha watoto na vijana wenzao kujiunga na vikundi hivyo.
Meneja Mawasiliano kutoka AGPAHI, Jane Shuma akielezea mambo mbalimbali yanayofanyika wakati wa kambi ya Ariel.
Watoto na vijana wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akimshukuru mgeni rasmi kwa kufungua kambi hiyo.
Kijana kutoka Geita akielezea kuhusu mchoro wa mti wa maisha unaoelezea historia yake fupi na malengo yake maishani.
Kijana akionesha mti wake wa maisha kwa mgeni rasmi.
Kijana mwenye ndoto za kuwa mwalimu bora kutoka mkoa wa Shinyanga akielezea kuhusu mti wake wa maisha kwa mgeni rasmi.
Kijana akionesha mkoba alioutengeneza kambini baada ya kufundishwa somo la stadi za maisha.
Watumishi wa afya walioambatana na watoto, wafanyakazi wa AGPAHI wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,Watumishi wa afya ,watoto na vijana.
Vijana na watoto wakicheza muziki kambini.
Watoto,vijana na walezi wao wakicheza.
Kulia ni waelimisha rika wakifurahia jambo na Watoto na vijana walioshinda katika shindano la Mkali Wao.Wamo waliopata ushindi kwa kujiamini,ucheshi,usikivu, utulivu,uchezaji mzuri wa muziki,kujibu maswali vizuri,uongozi mzuri,kutunza muda,nidhamu na utii na uchangamfu kambini.
Mkali wao kwa ucheshi.
Mkali wao kwa kuuliza maswali ya kidadisi.
Mkali wao kwa kucheza muziki vizuri.
Mkali wao kwa kujiamini.
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita ,Dk. Joseph Odero akitoa elimu kuhusu ufuasi mzuri wa dawa.
Washiriki wa kambi ya Ariel wakijadili katika kundi kuhusu elimu ya afya ya ujana na makuzi.
MATUKIO YALIYOJIRI SIKU YA KWANZA KAMBINI
Mtaalam wa Masuala ya Saikolojia kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando,Flora Swai akizungumza na watoto na vijana wanaoshiriki katika kambi ya Ariel 2017.
Meneja wa Huduma za Mama na Mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu akizungumza na washiriki wa kambi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la AGPAHI, Dk. Safila Telatela akitoa somo la lishe.
Dk.Telatela akiendelea kutoa somo la lishe.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Geita,Richard Kambarangwe akitoa maelekezo kuhusu kuchora mti wa maisha.
Kambarangwe akiendelea kutoa maelezo kuhusu mti wa maisha.
Mtumishi wa afya kutoka wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza,Joyce Nkinga akifuatilia kwa ukaribu jinsi watoto na vijana wanavyochora miti ya maisha yao.
Watoto na vijana wakichora miti ya maisha.
Vijana na watoto wakicheza kambini.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WATOTO NA VIJANA WA ARIEL CAMP WAKITEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA YA BUJORA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL JIJINI MWANZA
Bofya <<HAPA>> KUSOMA HABARI JINSI AGPAHI INAVYOENDELEA KUTOA HUDUMA YA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO TANZANIA
Bofya <<HAPA>> KUSOMA HABARI JINSI AGPAHI INAVYOENDELEA KUTOA HUDUMA YA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO TANZANIA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WATOTO NA VIJANA WA ARIEL CAMP WAKITEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA YA BUJORA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL JIJINI MWANZA
Bofya <<HAPA>> KUSOMA HABARI JINSI AGPAHI INAVYOENDELEA KUTOA HUDUMA YA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO TANZANIA
Bofya <<HAPA>> KUSOMA HABARI JINSI AGPAHI INAVYOENDELEA KUTOA HUDUMA YA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO TANZANIA
Social Plugin