Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Sandhya Rani (25) mkazi wa Kusini mwa nchini India ameuawa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake baada ya kukataa kuchumbiwa naye.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo, mashuhuda wa tukio hilo lililotokea siku ya Alhamis wanasema waliona mwanaume huyo akifuata mwanamke huyo na wakaanza kuzungumza kwa kubishana na ndipo mwanaume huyo alipochukua mafuta ya taa aliyokuwa ametembea nayo na kumwagia binti huyo kisha kumuwasha moto.
Inaelezwa kuwa watu walijaribu kumwokoa binti huyo lakini alikuwa ameungua sana na alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.
Inaelezwa pia kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi ofisi moja. Polisi jimboni humo tayari wamemkamata mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la Karthika Vanga.
Watu walikimbia kumsaidia bi Rani lakini alifariki akielekea hospitalini.
Mshukiwa huyo , Karthika Vanga , 28, ni mfanyikazi mwenzake wa zamani.
Alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na bi Rani hadi miezi michache iliopita, polisi liliambia ripota wa BBC Deepthi Bathini.
Wakati alipomkaribia siku ya Alhamisi wawili hao walionekana wakijibizana kabla ya mwanamume huyo kuchukua mafiua ya taa, na kumwagia mwilini na kumchoma moto , polisi walidai.
Walisema kuwa kulikuwa na madai kwamba bwana Vanga amekuwa akitaka kumchumbia bi Rani kwa kipindi cha miaka miwili.
Alikuwa amekataa mara kadhaa kuchumbiwa na bwana huyo ijapokuwa polisi wanasema haijulikani iwapo kulikuwa na malalamishi dhidi ya mtu huyo.
Mashambulizi dhidi ya wanawake nchini India yameongezeka tangu ubakaji wa gengi la mwaka 2012 na mauaji ya mwanafunzi katika basi moja mjini Delhi, na yamesababisha kuwekwa kwa sheria kali zinazolenga kukabiliana na mashambulio kama hayo.
Social Plugin