Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amekutana na wadau wa zao la pamba kutoka mikoa 16 inayolima pamba nchini.
Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa Desemba 22,2017 katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Savannah Plains iliyopo kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau wa pamba wakiwemo mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za wilaya,makatibu,wabunge,mashirika,taasisi na wadau mbalimbali.
Akizungumza katika hicho Waziri mkuu Kassim Majaliwa alisema kikao hicho kimelenga kupeana mikakati ya kuhakikisha zao la pamba linakuwa na mafanikio kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi.
Aliiagiza mikoa inayolima zao la pamba ‘dhahabu nyeupe’ kuelekeza nguvu katika zao hilo kuanzia kwenye maandilizi ya kilimo hadi masoko.
Majaliwa alisema serikali inataka zao la pamba ambalo uzalishaji ulidorora liwe na tija kwa uchumi wa taifa kwani zao hilo lina heshima na jina kubwa duniani hivyo viongozi wa mikoa na halmashauri za wilaya wahakikishe wanasimamia kikamilifu kilimo cha zao hilo.
“Jukumu la serikali sasa ni kusimamia kilimo mazao matano ambayo ni pamba,korosho,tumbaku,chai na kahawa,mazao haya tunataka kuyafanyia mikakati kuanzia kwenye kilimo hadi masoko na ninaendelea kukutana na wadau ili kupeana mikakati ya kuhakikisha kilimo cha mazao haya ikiwemo pamba yanakuwa na mafanikio”,alisema Majaliwa.
Pia aliziagiza halmashauri za wilaya kuwa na mpango kazi wa namna ya kufanikisha kilimo cha pamba na kwamba atafanya ziara kukagua mipango kazi hiyo na kuelezwa mafanikio yaliyofikiwa katika kila halmashauri.
Waziri mkuu aliwataka wataalamu wanaohusika na dawa na mbegu za pamba kutoa mbegu na dawa zinazotakiwa badala ya kuwavuruga wakulima kwa kuwapatia dawa na mbegu zinazofaa kwenye kilimo hicho.
“Tumechoka kusikia kuhusu dawa zisizoua wadudu,mara mbegu za manyoya,mara zenye vipara,tunachotaka sasa mtuambie ni dawa gani,mbegu gani zinafaa na siyo vinginevyo”,alisema Waziri Mkuu.
Aidha alizitaka halmashauri za wilaya kuhakikisha zinaachana na tabia ya kuhamasisha mikopo wakulima badala yake wawajengee uwezo wa kulima zao la pamba kwa njia za kisasa.
Katika hatua nyingine alieleza kusikitishwa na kukosekana kwa takwimu sahihi za wakulima wa pamba na kuagiza maeneo yanayolima pamba kuandaa takwimu.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Dr. Charles Tizeba alisema serikali imejipanga vyema katika msimu huu wa kilimo cha pamba na kwamba uzalishaji utaongezeka kwa asilimia zaidi ya 400.
Alisema hali ya hewa inaridhisha na tayari zoezi la kusambaza dawa na mbegu za pamba linaendelea hivyo msimu huu kilimo hicho kitakuwa na tija kutokana na wakulima kulima kwa njia za kisasa huku akishauri wakulima walime mbegu zisizo na manyoya.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog Kadama Malunde,ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kikao hicho
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa wakati akipokelewa na viongozi mbalimbali kuhudhuria kikao cha wadau wa pamba kutoka mikoa 16 nchini katika ukumbi wa shule ya sekondari Savannah Plains. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ukumbi wa shule ya sekondari Savannah Plains.Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akifuatiwa na Waziri wa Kilimo Dr. Charles Tizeba.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifuatiwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Wajumbe wakimpokea waziri mkuu ukumbini na kuimba wimbo wa taifa
Wakuu wa mikoa wakiwa ukumbini
Wadau wa pamba wakiwa ukumbini
Wadau wa pamba wakiwa ukumbini.Kushoto ni wakuu wa wilaya,kulia ni wakuu wa mikoa
Wadau wa pamba wakiwa ukumbini
Wakuu wa mikoa wakiwa ukumbini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa pamba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza ukumbini
Waziri wa Kilimo Dr. Charles Tizeba akizungumza katika kikao hicho
Wakuu wa wilaya wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Wajumbe wakiwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Viongozi wa vyama vya siasa nao walikuwepo
Wadau wa pamba wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin