Shirika la Kivulini limeendesha mdahalo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wana mabadiliko kutoka kata ya Nyida,Nsalala na Itwangi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mdahalo huo pia umehudhuriwa na wana mabadiliko kwa njia ya Mitandao ya Kijamii (Bloggers) katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mdahalo huo umefanyika leo Ijumaa Machi 30,2018 katika ukumbi wa Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Tinde ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Muhoja.
Akizungumza wakati wa mdahalo huo,Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Muhoja alisema matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yamepungua katika kata ambazo shirika la Kivulini limetoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia kupitia wana mabadiliko.
"Tulichovuna kutoka Kivulini ni mabadiliko kwenye kata za kata ya Nyida,Nsalala na Itwangi,niwakumbushe tu kuwa mabadiliko katika jamii ni endelevu na yanahitaji nguvu ya pamoja,lazima kwanza uanze kwa kubadilika wewe mwenyewe kisha wengine wanafuatia",alieleza Muhoja.
Hata hivyo alisema bado kuna mfumo dume katika suala la umiliki wa ardhi kwani wanawake hawapewi haki ya kumiliki ardhi hivyo elimu inatakiwa kuendelea kutolewa kwa jamii.
Aidha Muhoja aliwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika jamii pale nafasi inapotokea ili kufikia usawa wa 50% kwa 50%.
Alisema katika halmashauri ya Shinyanga yenye vijiji 126 viongozi wanawake ni watatu pekee huku wanawake waliochaguliwa kuwa madiwani ni wawili pekee katika kata 26 zilizopo katika halmashauri hiyo.
Meneja wa Kampeni ya Mradi wa ‘Tunaweza’,unaofadhiliwa na shirika la Oxfam, Eunice Mayengela kutoka shirika la Kivulini,alisema mdahalo huo umelenga kujadili changamoto na mafanikio yaliyofikiwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wao,washiriki wa mdahalo huo wakiwemo wana mabadiliko kupitia njia ya mitandao ya kijamii walisema matukio ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake yanaendelea kupungua kutokana na jamii kuelimishwa juu ya madhara ya ukatili.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsalala,Sandeko Ndegeleja alisema kupitia elimu inayotolewa na shirika la Kivulini hivi sasa katika kijiji chake wazazi wanapotaka kuozesha watoto wao wamekuwa wakifika kwenye uongozi wa kijiji na kuuliza kama binti zao wanafaa kuozeshwa au la.
Naye Monica Simon alisema ukatili uliopo kwenye maeneo mengi katika wilaya ya Shinyanga ni ukatili wa kiuchumi ambao wanaume huwa na sauti zaidi ya umiliki wa mali za familia kuliko wanawake.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Muhoja akizungumza wakati wa mdahalo kuhusu ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la Kivulini kwa ufadhili wa shirika la Oxfam
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Muhoja akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Asha Omari akizungumza wakati wa mdahalo huo ambapo alisema pamoja na matukio ya ukatili kupungua bado mila na desturi zinachangia kuwepo kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Meneja wa Kampeni ya Mradi wa ‘Tunaweza’,unaofadhiliwa na shirika la Oxfam, Eunice Mayengela kutoka shirika la Kivulini akiongoza mdahalo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Wana mabadiliko kutoka kata ya Nyida,Nsalala na Itwangi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Tinde wakati wa mdahalo.
Wana mabadiliko kwa njia ya mitandao ya kijamii ambao ni bloggers kutoka jijini Dar es salaam wakiwa ukumbini.
Afisa Mtendaji kata ya Nyida David Lazaro akichangia hoja wakati wa mdahalo ambapo alisema matukio ya wanafunzi kupewa mimba yamepungua kutokana na watoto/wanafunzi kupelekwa shule.
Mwana Mabadiliko Monica Simon akichangia hoja wakati wa mdahalo ambapo alisema wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto ya ukatili wa kisaikolojia hivyo kusababisha waone aibu kusema pale wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsalala Sandeko Ndegeleja akizungumza wakati wa mdahalo huo. Alisema hivi sasa jamii imebadilika kutokana elimu inayoendelea kutolewa katika jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara
Mwenyekiti wa kijiji cha Welezo Janeth Mabula akichangia hoja wakati wa mdahalo huo ambapo aliwataka wanawake kutokaa kimya wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.
Mwana mabadiliko James Masunga kutoka Itwangi akichangia hoja wakati wa kujadili kuhusu ukatili wa kijinsia.
Kushoto ni Meneja wa Kampeni ya Mradi wa ‘Tunaweza’,unaofadhiliwa na shirika la Oxfam, Eunice Mayengela kutoka shirika la Kivulini akisikiliza hoja kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nsalala Jacob Jomanga.
Mzee Joseph Maganga kutoka kata ya Itwangi akielezea kuhusu masuala ya umiliki wa mali katika familia ambapo wanawake wengi wanachangia kuwepo kwa ukatili kutokana na kutokuwa tayari kutumia na mali zao badala yake wanataka mali za wanaume tu ndiyo zitumike katika familia.
Eunice Mayengela akiendelea kuongoza mdahalo.
Mwana Mabadiliko kwa njia ya Mitandao ya Kijamii Krants Mwantepele akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Mwana mabadiliko Elizabeth Richard akielezea kuhusu vitendo vya kikatili.
Mwana Mabadiliko kwa njia ya mitandao ya Kijamii Veronica Ignatius akichangia hoja wakati wa mdahalo huo.
Mwana Mabadiliko kwa njia ya mitandao ya kijamii akichangia hoja wakati wa mdahalo huo.
Washiriki wa mdahalo wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog