HUAWEI YATOA WITO WA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA ZA UMMA, BINAFSI

Rais na mwanachama wa bodi ya wakurugenzi ya Huawei, Catherine Chen
**
Na Mwandishi wetu

Kampuni ya mawasiliano ya China ya Huawei imetoa wito wa uwepo wa ushirikiano madhubuti baina ya sekta za umma na sekta binafsi ili kurejesha imani baina ya sekta hizo mbili kwa mustakabali mzima wa uboreshaji wa teknolojia.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Makamu Mwandamizi wa Rais na mwanachama wa bodi ya wakurugenzi ya Huawei, Catherine Chen kwenye  Kongamano la Mtakatifu Gallen - mkusanyiko wa viongozi wa sasa na wa baadaye kutoka kote ulimwenguni ambao hufanyika kila mwaka.

Kongamano hilo lililenga kusherehekea kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Katika kongamano hilo, jumla ya watu 1,000 walishiriki kwenye mazungumzo ya siku tatu baina ya vizazi tofauti kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Gallen, kituo cha kimataifa Singapore, Balozi kumi za Uswizi kote ulimwenguni, na mahali pengine mtandaoni.

Wasemaji wengine kwenye kongamano hilo ni pamoja wakuu mbalimbali kutoka sekta binafsi ambao ni pamoja na Christophe Franz, Mwenyekiti wa bodi ya Roche, Ola Källenius, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi huko Daimler, Satya Nadella, Afisa Mtendaji Mkuu wa Microsoft, na Roshni Nadar Malhotra, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la HCL.

Washiriki, ambao pia walijumuisha viongozi wa kisiasa, kama vile Kansela wa Austria, Sebastian Kurz, na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, kama Mwenyekiti wa mpango wa kidijitali Uswizi, Doris Leuthard, walikusanyika kubadilishana maoni yao juu ya mada ya kongamano la mwaka huu, "Uaminifu ni Muhimu" kitu ambacho Huawei imejitolea sana.

Kwa mujibu wa Chen anaamini inahitajika juhudi za pamoja za watunga sera, wasimamizi, na sekta binafsi. "Kwa kuwa vifaa vingi vinajumuisha mawasiliano, uwepo wa ongezeko la huduma kwa njia za mitandao pamoja na miundombinu muhimu kutegemea upatikanaji wa data kwa wakati halisi, ni lazima kwa serikali zote ulimwenguni kuhakikisha kuwa kila mtu analindwa kwa kiwango cha juu kabisa kiusalama. Kitu pekee kinachoweza kuleta imani katika teknolojia ni uwepo wa sheria moja na jumuishi kwa nchi zote,” alisema.

Kongamano hilo kwa mwaka huu lilianza Mei 5. Washiriki wa hafla hiyo walikubaliana kwamba uaminifu hujengwa kwa uwazi, na kwamba ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia changamoto hiyo na hatari ambazo zimeibuka baada ya janga la COVID-19.

Uaminifu wa umma katika taasisi za kisiasa na kiuchumi, teknolojia zinazoibuka, na vyombo vya habari vimeharibiwa hivi karibuni, haswa kati ya kizazi cha vijana, na hii imezidishwa na janga la COVID-19.

"Sisi, kwa kizazi chetu, tunaunganishwa na idadi kubwa ya watu kupitia mitandao ya kijamii, lakini hii haimaanishi ni kundi la watu ambao tunaweza kuwaamini," alisema Simon Zulliger, mshiriki wa timu ya wanafunzi 35 kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Gallen ambacho kiliandaa kongamano la mwaka huu. Timu hiyo ilielezea maoni yao kuwa kutafuta njia za kuhifadhi na kuimarisha uaminifu ni muhimu kwa kurudisha imani.

Chen anatumaini kwamba kizazi kijacho cha viongozi kitaunda uaminifu na kuunda ulimwengu uliounganishwa kimtandao. "Ninawahimiza waendelee kukuza uhusiano mzuri kati ya jamii, watu, na mazingira yao. Lazima tujenge imani kubwa katika teknolojia, iliyowezeshwa na ya sheria jumuishi, ubunifu na maendeleo. Hapo tu ndipo tunaweza kujitolea kwa matumizi endelevu na ya kuaminika ya teknolojia," alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments