AJINYONGA BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA MKEWE

HATARI: AJINYONGA BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA MKEWE


Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mkazi wa mtaa wa Mpanda hotel wilaya yam panda mkoa wa katavi Nzego Vicent (33) amejiua  kwa kujinyonga na kamba baada ya mkewe kumnyima tendo la ndoa.
Tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 7:30 usiku jirani na nyumba waliokuwa wakiishi wanandoa hao.
Mke wa marehemu huyo aitwaye Agnes Nicodemu alisema siku hiyo ya tukio hilo mumewe ambaye alikuwa ametoka kwenye pombe za kienyeji alifika nyumbani kwake majira ya  saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe tendo la ndoa.
Alisema kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana alimwomba mumewe avumilie hadi siku itakayofuata kwa kile alichomweleza kuwa hakuwa tayari kufanya nae tendo landoa kwa kuwa alikuwa amechoka.
Baada ya marehemu Nzego kujibiwa hivyo hakuridhika nna kauli hiyo ya mkewe na ndipo alipoanza kumshutumu kuwa huenda ana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.
Ndipo Nzego alipoamua kuanza kumshambulia mkewe huyo kwa kumpiga kichapo huku akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa panga.
Agnes baada ya kuona kipigo kimezidi aliamua kukimbia nje ili kukwepa kipigo alicho kuwa akichapwa na mumewe.
Baada ya mkewe kukimbia marehemu aliamua kutoka nje huku akiwa na shoka mbili na kuelekea kusiko julikana na kuacha nyumba yake ikiwa wazi.
Ndipo majira ya ssa 12:30 asubuhi mkewe na marehemu alipofuatwa na majirani na walimweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi.
Mkewe huyo aliamua kufuatana na majirani hao hadi kwenye eneo hilo na ndipo alipomwona mumewe akiwa amening’inia juu ya mti akiwa amekata roho.
Kamanda wa polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mtu kujinyonga kwa kutumia kamba katika mtaa huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post