Dk Stephen Ulimboka
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka leo ameeleza ya
moyoni baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia kwa
wanasheria wake ambao ni Shayo na Nyaroro Kichere. Taarifa hiyo
imeeleza kuwa aliyekuwa anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa,
kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na
hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu
ni Bwana Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa na baadhi ya vyombo vya
habari kuwa ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Katika taarifa
hiyo Dk. Ulimboka anaeleza kushangazwa na kutokamatwa mtu huyo mpaka
sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru japo
mpaka sasa haijaundwa.
Chanzo: Kilimanjaro Blog
Social Plugin