Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe
JESHI
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi kuepuka vurugu
zinazohatarisha usalama, na kulinda amani iliyopo nchini
JWTZ
imetoa kauli hiyo siku moja baada ya waumini wa dini ya Kiislamu
jijini Dar es Salaam kuandamana sababu ya malalamiko kadhaa kama
kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 wiki iliyopita kwa
tuhuma mbalimbali, kutoweka kwa kiongozi wa UAMSHO Sheikh Amir Farid
Hadi, na malalamiko mengine.
Msemaji
wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, amesema hatua ya wanajeshi kujitokeza
katika kuzima vurugu zilizotokea jijini juzi, ilikua na lengo la
kuwaonyesha wananchi kwamba JWTZ ipo kikazi zaidi, na anayetaka vurugu
atashughulikiwa kisheria.
“Juzi
tulionyesha ‘talent show force’ ili watujue kama tupo kazini, hata
kama wametuona tupo kimya, hatuna mzaha katika kulinda na kusimamia
ulinzi na usalama wa taifa hili, kwa hiyo tulikuwa kwenye sehemu ya
utekelezaji wa majukumu yetu, na kwamba atakayekwenda kinyume
tutamshughulikia,” alisema Mgawe.
Alisema
zoezi hilo litaendelea kwa maandamano yoyote yatakayoonyesha dalili za
kuhatarisha usalama wa nchi. Aliongeza kwamba wanajeshi watashiriki
kikamilifu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafuata sheria na taratibu
zilizopangwa, bila ya kuathiri usalama wa nchi.
Alisema
kwa sasa wanasubiri kibali cha polisi cha kuhusu kuhitaji msaada ili
waweze kuungana nao katika kushughulikia maandamano yenye lengo la
kuhatarisha amani na utulivu.
“Tunawataka
wananchi kufuata sheria na taratibu zilizopo na kuepuka kuhatarisha
amani ya nchi, kama wanataka tuingie kazini tutafanya hivyo, ila
tunachowaasa ni kufuata taratibu zilizopo,” alisisitiza.
Katika vurugu za juzi, watu 53 walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, watu hao
watafikishwa mahakamani Oktoba 22 mwaka huu. Source: Mdimuz blog
Social Plugin