Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wanaotumia silaha wameuawa kwa kuchomwa kwa moto na wananchi wa vijiji vya Ibanza na Sumbigu katika wilaya ya Shinyanga vijijini baada ya kuvamia,kupora kwa nguvu,kujeruhi na kuwabaka wanawake watatu wakazi wa kijiji cha Shatimba wilayani humo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,ambapo amesema majambazi hao waliuawa usiku wa kuamkia tarehe 18 Octoba 2012 na kuwataja waliouawa kuwa ni Emmanuel Faustine(39) mkazi wa Kabuhima Runzewe Wilayani Geita,Mkoani Geita na mwingine aliyejulikana kwa jinamoja la Mathias mkazi wa kijiji cha Shatimba pamoja na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Dokta.
Amesema Katika tukio hilo majambazi wengine watatu walifanikiwa kutoroka,na juhudi za kuwasaka bado zinaendelea.
Walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa,baada ya majambazi hao kuvamia kijiji cha Shatimba majira ya saa 10 alfajiri,majambazi hao waliingia katika nyumba za familia tatu tofauti,ambapo walifanikiwa kupora simu nne za mkononi zenye thamani ya shilingi laki saba na 30 elfu.
Aidha mbali na kupora vitu hivyo,pia walimjeruhi kwa kumkata mapanga mtu mmoja na baadaye kuwabaka wanawake watatu mbele za waume zao.
Social Plugin