Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MLINZI AVAMIWA NA MAJAMBAZI,NA KUJERUHIWA ,ALIKUWA NA BUNDUKI AINA YA SHORTGUN ,RISASI KAWEKA MFUKONI-SHINYANGA

Watu wasiojulikana wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamemvamia mlinzi wa kampuni ya SESEKO  wakati akiwa katika lindo lake la EXPORT TRADING CO.LTD katika Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga jana usiku majira ya saa mbili kasoro dakika 20.

Imeelezwa kuwa mlinzi huyo aitwaye Edward Mayunga(38) mkazi wa Mtaa wa Viwandani akiwa katika lindo lake alivamiwa na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na mapanga na marungu,na kisha kumjeruhi kwa panga kwenye kisogo na kumnyang'anya bunduki aina ya Shortgun  yenye namba 05018378,ambayo haikuwa na risasi,mali ya kampuni hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,ambapo amesema mlinzi huyo wa kampuni ya SESEKO alifanikiwa kuokoa risasi 4 za Shortgun alizokuwa nazo katika sare zake za kazi.

Kamanda Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali ambapo majeruhi amelzwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na juhudi za kuwatafuta watuhumiwa zinaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com