Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAFUNZI MWAKA WA KWANZA UDSM AJINYONGA.


Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza  Chuo kikuu cha Dar es Salaam  ameamua kujinyonga kwa kutumia nguo zake  ,katika  nyumba moja ya kulala wageni jijini Dar es salaam
Kwa mujibu wa  mkoa wa kipolisi wilaya ya Kinondoni bw Charles Kenyela amesema  mwanafunzi  aliyefahamika kwa jina Joseph Lugemalila, {21}, aliamua kujiuwa  katika nyumba ya kulala wageni iliyofahamika kwa jina  Rombo Guest House katika eneo la manzese jijini hapa ikiwa ni siku  sita zimepita tangu aripoti katika chuo hicho.
Kamanda Kenyela amesema  mwili wa Lugemalila, ambaye anatokea  katika wilaya ya Ukerewe mkoa wa  Mwanza Region, umekutwa siku ya ijumaa , katika nyumba hiyo  huku akiwa amejiandikisha kwa jina la  Dickson John.

Katika upekuzi  uliofanywa na jeshi la polisi  umekuta  vifaa mbalimbali vya shule pamoja na ujumbe aliokuwa ameandikwa  kijana huyo unaosema ‘Nimeamua  kujiuwa  kutokana  na namba kubwa ya matatizo niliyonayo’
Moja ya vifaa ya shule vilivyokutwa  kwenye chumba hicho  ni pamoja na cheti cha afya alichokuwa amewpimia afya yake kwa ajili ysa kujiunga na chuo hicho  katika hospitali ya chuo kikuu cha Dar es salaam cheti ambacho kilionyesha ya Lugemalila  akiwa ambukizwa  virusi vya ugonjwa wa UKIMWI {HIV-positive}

Msemaji wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam BW Jackson Isidory AMETHIBITISHA KUWA Joseph Lugemalila, alikua mwanafunzi halali wa chuo hicho.
Kwa upande wake baba wa mwanafunzi huyo bw  Pastory Lugemalila, ambaye alikuwa safarini kuja  Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukuwa mwili wa kijana wake licha ya kukiri kushtushwa na taarifa hizo amesema kuwa mwanae huyo alimpigia simu wiki moja iliyopita kabla ya kifo chake na kumwambia kwamba  amefanikiwa kukamilisha mambo yake ya kimasomo

Mwili wa kijana huyo umesafirishwa kuelekea mwanza  kwa ajili ya maziko .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com