Mwandishi wa Syria na mtafiti wa kisiasa, aliyejulikana kwa maandisi
yake makali ya kuchochea kupinga Uyahudi, ameuwawa kwa
kuteswa na usalama wa taifa wa Syria.
Taarifa ya kifo hicho ni kwa
mujibu wa familia yake na vikundi vya upinzani. Mohammed Nimr al-Madani,
aliyekuwa na umri wa miaka 51, aliuwawa siku 10 zilizopita
lakini mpaka sasa mwili wake bado upo katika mikono ya maafisa wa
ujasusi wa Syria.
Mwandishi huyo aliyekuwa baba wa watoto watatu
aliwahi kukamatwa mara tatu na maafisa usalama wa taifa tangu
kuanza kwa vuguvugu la mageuzi la kumpinga Rais Bashar al-Assad
Machi 2011.
Makundi ya wanaharakati wanasema Nimr alikuwa
mwakilishi wa siri wa vyombo vya habari vya kigeni nchini humo.
Katika ukurasa wake wa facebook marehemu amejielezea kuwa ni
mtaalamu wa masuala ya dini na maangamizi ya Wayahudi, tukio
ambalo amelikanusha vikali katika maisha yake yote.
Social Plugin