Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Mwawaza katika Manispaaa ya Shinyanga bwana Bundala Katunge amejeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa mkuki tumboni na watu wasiojulikna usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema mwenyekiti huyo wa chadema akiwa amelala nyumbani kwake majira ya saa tano alisikia kelele za watu nje ya nyumba yake na baada ya kutoka nje alikuta kundi la watu wakishusha bendera ya chama hicho iliyotundikwa hapo na waliomuona wakakimbia na mmoja wao kumchoma na mkuki ubavuni.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa Dr Fredrick Mlekwa amesema wamempokea majeruhi huyo na kumfanyia oparesheni na hali yake amesema inaendelea vizuri.
Social Plugin