Ulimboka Kutaja Wabaya Wake ...!
KIONGOZI
wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, amepanga kumwaga
taarifa nyeti kuhusu kutekwa na kuteswa kwake na kisha kutupwa katika
Msitu wa Mabwepande, Bunju, jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa ndugu na rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka, ameliambia Mwananchi kuwa,
kiongozi huyo wa jumuiya, amepanga kuanika hayo katika mkutano wake na
waandishi wa habari. Alisema Dk Ulimboka, atatumia mkutano huo kueleza
siri ya kutekwa kwake.
“Siku
yoyote kuanzia sasa umma, utafahamu ukweli halisi wa kilichompata
kijana wetu. Niliongea naye juzi na amenithibitishia kuwa atakutana na
waandishi wa habari na kueleza kila kitu katika masahiba yaliompata,”
alisema ndugu huyo wa Ulimboka ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake
litajwe gazetini.
Alisisitiza
“Ni kweli kwamba Steven (Dk. Steven Ulimboka) amepanga kukutana na
waandishi wa habari. Anataka kutumia mkutano huo, kuanika wote
walioshiriki kumtesa, kumteka na kisha kumtupa katika msitu wa
Mabwepande,” Alipoulizwa kuhusu kipya ambacho daktari huyo ataueleleza
ulimwengu ambacho hakijafahamika, mwanafamilia huyo alisema:
“Tuvute
subira. Steven amepanga kutaja wote waliohusika katika kutaka
kuangamiza maisha yake. Ameniambia kuwa anataka kuwaambia Watanzania
ukweli wa kilichompata,” Dk Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26 mwaka
huu, katika maeneo ya Leaders Club jijini Dar es Salaam na baadaye
kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikononi na miguuni kabla ya
kunyofolewa kucha na meno; katika Msitu wa Mabwepande.
Aliokotwa
na wasamaria wema asubuhi yake na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Juni 30
kwa matibabu zaidi. Tangu aliporejea nchini Agosti 12 mwaka huu,
kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka ndani na nje ya nchi, kumtaka
azungumze kwa madai kuwa kauli yake itasaidia kujulikana kwa ukweli
kuhusu kilichompata. Kufanyika kwa mkutano huo kunatajwa na wachambuzi
wa mambo kuwa kunaweza kuondoa kiwingu hicho, ikiwa ni pamoja na kujibu
baadhi ya maswali yaliyobuka juu ya tukio hilo.
mahojiano
yake ya kwanza na gazeti hili, wiki iliyopita, Dk. Ulimboka alisema
hali yake inaendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba anamshukuru
Mungu na wote waliomuombea, ingawa bado anahitaji matibabu zaidi.
“Madaktari
wangu bado wanaendelea na uchunguzi kuhusu figo zangu ili waone kama
zinaweza kufanya kazi au zinahitaji kuondolewa na kuwekwa nyingine.
Lakini kwa jumla, hali yangu inaleta matumaini kidogo.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Social Plugin