Huyu ndiye Mohammed Iqbal Dar , aliyebuni jina la Tanzania |
UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru.
Hata hivyo,
katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu
waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine,
michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye
historia hizo.
Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi
yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa
moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa
shuleni.
Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.
Lakini
ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi
walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Mohammed Iqbal Dar ndiye
aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.
Ilikuwaje?
“Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo,” anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza:
“Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichuka karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote.”

“Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika
na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya,”
anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na
Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.
Kupata jina Tanzania
Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.
“Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,”anasimulia Dar.
“Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,”anasimulia Dar.
Anabainisha
kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika
yanaishia na IA mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia,
Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini
hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.
“NIlituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani,” anasema Dar.
Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.
“Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda,

“Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi
alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa
akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini,
nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi
sana,” anaeleza.
Tuzo
Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.
Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.
Pamoja
na kuibuka mshindi wa ubunifu huo na hadi leo jina la Tanzania
alilolibuni yeye linaendelea kutumika, lakini Dar anadai kuwa mchango
wake huo kwa taifa ni kama hautambuliwi na Serikali imemsahau katika
kuandika historia ya taifa la Tanzania.
“Sijui kwa nini
sitambuliwi tangu wakati huo? Hakuna chochote kinachoelezea uhusika
wangu katika kupata jina la Tanzania na ukiwauliza watu, wengi
watakwambia ilikuwa ni Nyerere aliyeleta jina Tanzania, hii inaumiza,”
anasema akilalamika.
Tanzania ya sasa
Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere, Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani.
Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere, Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani.
“Ni
kama imepita miaka mingi sana tangu kifo chake. Watanzania wamesahau
kila kitu alichokiota Mwalimu Nyerere. Nakumbuka moja ya vita kubwa
aliyopigana ni dhidi ya rushwa, yeye aliichuki rushwa lakini kwa sasa,
rushwa imekua kama ndiyo tafsiri ya maisha ya Tanzania. Hakuna kitu
kinachoweza kufanyika kwa urahisi hata kama ni haki ya mtu, bila kutoa
rushwa,” anasema.
Anaongeza kuwa: “Mwalimu Nyerere alikua ni
rafiki ya baba yangu na walikua wakionana na kuongea, nakumbuka siku
moja kulikuwa na sherehe nyumbani na kwa kuwa tulikuwa watoto,
nilimhudumia chai Mwalimu.
“Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumuuliza
baba yangu; Lini Malaria itaisha nchini hii? Baba alimjibu kuwa, kamwe
malaria haitaisha ikiwa hakutakuwa na kujitolea kwa kila mmoja wetu,
bila kumtegea mwengine,” anasema.
Katika kumbukumbu ya kifo cha
Baba wa Taifa, Dar anaishauri Tanzania iendeleze misingi ya maisha
ambayo Hayati Mwalimu Nyerere aliisimmamia, ikiwamo umoja na
mashikamano, ili kuondoa tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri.
“Tunaona
namna ambavyo matajiri wanendelea kuwa tajiri zaidi, wakati maskini
wanazidi kudidimia. Kama kungekuwa na ushirikiano kati ya watu hawa
wawili, tofauti kati yao ingekuwa ndogo au isingekuepo kabisa,”
anaeleza.
Anashauri pia kuwepo na sanamu za utambulisho ya Baba wa
Taifa kila mahali, ili kulienzi jina lake liishi milele. “Kwa
ninavyomjua Mwalimu natamani jina lake liishi milele na litangazwe
lijulikane dunia nzima,”anasema.
Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar.
Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar.
Dar
ni baba wa mtoto mmoja, ambapo kwa zaidi ya miaka 40 sasa amekuwa
akiishi nchini Uingereza alikoenda kwa ajili ya kusoma kabla ya kuwa
raia wa nchi hiyo.
Mbunifu huyo wa jina la Tanzania ni Mhandisi wa
Masuala ya Redio, kazi anayoifanya nchini Uingereza, akieleza kuwa
katika kuienzi nchi yake, nyumba yake iliyopo mjini Birmingham, ameipa
jina la Dar es Salaam, ikiwakilisha ubini wake, pamoja na Jiji la Dar es
Salaam.
Chanzo: Mwananchi
Social Plugin