Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKAZI WA ISANGA MBEYA WAGOMA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDI WAAMUA KWENDA KUFANYA USAFI MAKABURI YA ISANGA


Wakazi wa isanga jijini mbeya  wamesema sherehe yao leo ni kufanya usafi katika makaburi ya isanga ilikuondoa vichaka vyote na kuchoma moto kuepuka vibaka na wavuta bangi wanaojificha makaburini hapo pia wameomba halmashauri ya jiji kuweka watu wa kufanya usafi kwani hilo eneo ni lao jiji
Wakiongea na Mbeya yetu wakazi hao wa isanga wamesema leo hawasherehekei sikukuu ya idi badala yake leo sherehe yao ni kufanya usafi katika makaburi ya isanga na zoezi hili litaendelea kila jumaosi na siku za mapumziko mpaka makaburi hayo yawe safi kabisa
Hakika wazee wengi na vijana wamejitokeza katika kufanya usafi katika makaburi haya ya isanga
Mzee mbio akiwahi kufanya usafi kweli leo wamegoma kusherehekea Idi

Bibi nae hakucheza mbali na eneo la tukio hataki mchezo yupo kukwatua visiki vidogodogo hapo makaburini
Bibi sasa amechoka anasaidiwa jembe
Watangazaji wa Bomba FM Gabriel na Kamanga matukio nao waliungana na wakazi hao wa isanga katika kufanya usafi wa makaburi hayo ya isanga 
Joseph mwaisango wa mbeya yetu hakucheza mbali natukio hilo nae akifanya usafi kuwakilisha Tone Multimedia company Limited
Kwa sasa hali ndiyo inaonekana hivi na usafi unazidi kuendelea hapa katika makaburi ya isanga
Haya maeneo bado yataendelea kufyekwa
Baadhi ya watu wanaendelea kuja na kuhamasika toka sehemu mbalimbali za jiji mara baada ya kusikia wenzao wa isanga wapo kufanya usafi katika makaburi ya isanga Bomba FM nayo ipo live makaburini hapa kuwahamasisha wakazi wa mbeya kuja fanya usafi makaburi ya isanga
Wenye kuleta maji haya chai sawa yaani ni raha tu hapa makaburini


Source: mbeyayetu.blogspot.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com