ASKOFU ALOYSIUS BALINA WA JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA AFARIKI DUNIA
Tuesday, November 06, 2012
Enzi za Uhai wake
Waziri
Mkuu, akiwa na Askofu Balina katika Ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo la Bunda
iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda
Februari 20, 2011.
MHASHAMU ASKOFU ALOYSIUS BALINA AMEFARIKI DUNIA LEO SAA TANO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO ALIKOKUWA ANAPATIWA MATIBABU KUTOKANA NA UGONJWA WA SARATANI YA INI.KWA MUJIBU WA TAARIFA KUTOKA KATIKA JOPO LA WASHAURI WA ASKOFU JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA KESHO ITAFANYIKA MISA YA KUMWOMBEA MAREHEMU SAA KUMI JIONI KATIKA KANISA LA MAMA MWENYE HURUMA LILILOPO NGOKOLO MJINI SHINYANGA AMBAPO MAZISHI YATAFANYIKA TAREHE 11 SIKU YA JUMAMOSI WIKI HII SAA NNE ASUBUHI KATIKA KANISA LA MAMA MWENYE HURUMA,NGOKOLO MJINI SHINYANGA.
MAREHEMU
ASKOFU BALINA ALIZALIWA JUNI 21 MWAKA 1945 HUKO ISOSO WILAYANI BARIADI MKOA
MPYA WA SIMIYU.
ALIPEWA
DARAJA TAKATIFU YA UPADRI JUNI 27 MWAKA 1971 AMBAPO MWAKA 1984 ALITEULIWA KUWA
ASKOFU WA KWANZA WA JIMBO KATOLIKI LA GEITA NA BABA MTAKATIFU PAPA YOHANE PAULO
WA PILI.
ALISIMIKWA
RASMI KUWA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA GEITA JANUARI 06 MWAKA 1985 NA BAADAYE
MWAKA 1997 ALITEULIWA KUWA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA KUFUATIA KIFO
CHA ALIYEKUWA ASKOFU WA SHINYANGA MAREHEMU CASTORY SEKWA.
Rais
Kikwete aomboleza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumanne, Novemba 6, 2012, amelitumia Kanisa Katoliki Tanzania salamu za
rambirambi kuomboleza kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu
Baba Askofu Aloysius Balina aliyefariki dunia majira ya saa tano asubuhi leo
kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.
Katika salamu zake za rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mshahamu Baba
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa
mshtuko mkubwa
taarifa za kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina ambaye nimeambiwa
ameaga dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Buganda, Mwanza, kwa
ugonjwa wa kansa.”
AmesemaRais Kikwete katika salamu zake hizo: “Mhashamu Baba Askofu Balina
alikuwa
kiongozi hodari na mwadilifu ambaye siyo tu alichangia kipekee katika mwenendo
mzuri
wa kiroho wa waumini wa Kanisa Katoliki bali pia katika maendeleo ya Watanzania
wote kwa jumla.”
“Kifochake kimetuondolea kiongozi mwema ambaye tutazikosa busara zake na uongozi
wake. Lakini napenda kukuhakishia Mshahamu Baba Askofu kuwa sisi ndani ya
Serikali tutaendelea kutambua na kuthamini mchango wa Askofu Balina alioutoa
kwa nchi yetu katika maisha yake,”
amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“BabaAskofu, nakuomba upokee salamu za rambirambi za Serikali ninayoiongoza na zangu
binafsi kufuatia msiba huu mkubwa. Aidha, kupitia kwako, naomba uwafikishie
salamu zangu viongozi na waumini wote wa Kanisa Katoliki kwa kuondokewa na
kiongozi na muumini mwenzao. Naungana nanyi kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema, aiweka pema peponi roho ya Marehemu. Amen.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2012
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin