Bakhresa (kulia) alipokuwa akisalimiana na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein
Orodha
ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa
jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania.
Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30
kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola
milioni 520 hadi kufikia November, 2012.
Bakhresa
ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza
kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga
wa kusaga.
Leo
hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa
zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi
ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta
miongoni mwa nyingine.
Kampuni
ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika
Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric.
Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo
mbalimbali.
Angalia list nzima hapa:
Social Plugin