Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbrod Slaa
--
Na Edson Kamukara
SIKU
moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete,
kuwataka makada wa chama hicho kujibu mapigo ya wapinzani,akidai
wanafanya kazi ya kueneza uongo na kupotosha wananchi, CHADEMA imesema
inamvutia pumzi kabla ya kumjibu.Akihitimisha mkutano mkuu wa CCM
mjini Dodoma juzi usiku, Rais Kikwete aliwataka mawaziri na makada wa
chama hicho kufanya mikutano ya hadhara na kutumia vyombo vya habari
kujibu hoja za wapinzani badala ya kutegemea nguvu za Jeshi la
Polisi.Huku akionekana kukasirishwa na kasi ya CHADEMA, Rais Kikwete
alimtaja wazi wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kuwa
aliwahi kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.
“Slaa
aliita mkutano akasema mimi, mwanangu Ridhiwani na Rostam Aziz
tulikutana kwenye hoteli moja jijini Mwanza, huku akijua siku aliyoitaja
mi nilikuwa kusini nikiendelea na shughuli zangu,”alisema.
Rais
Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya upinzani,watu wazima
hovyo,wanasema uongo mbele wananchi na hata wakati mwingine kwenye
vyombo vya habari wakinukuu takwimu za uzushi.
Alipoulizwa jana
kuhusu madai hayo ya kueneza uongo kwa wananchi,Dk.Slaa alicheka kisha
akasema:“Tunawatafakari na tutawajibu,ila siyo leo, wala hatuna
haraka.“Mimi kwa kweli sikusikiliza hotuba yake, na hata mkutano wa CCM
sijaufuatilia, ila kama Kikwete kasema hayo unayoniuliza, basi
tutamjibu kwa utaratibu rasmi wa chama, leo sisemi kitu.
“Sisi ni watu makini, tunaamini katika kile tunachokisema wala wasipaniki, tutawajibu.
Maana wanadhani tunapoteza muda kufuatilia mkutano wao,nilimsikia hata Nape Nnauye akisema juzi kuwa anajua tumeacha kazi tunawakodolea macho,”alisema.
Maana wanadhani tunapoteza muda kufuatilia mkutano wao,nilimsikia hata Nape Nnauye akisema juzi kuwa anajua tumeacha kazi tunawakodolea macho,”alisema.
Dk.Slaa
alisema kauli ya Nape ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri
Kuu(NEC),Itikadi na Uenezi wa CCM,inachekesha, kwani CCM ya wao kuacha
kazi zao na kuikodolea macho ilikuwa ya zamani si hii ya leo.
Katika
kile kinachoonekana kama CHADEMA kuinyima usingizi serikali na CCM,
Kikwete aliagiza mawaziri wote kujiwekea utaratibu wa kila mmoja kutoa
taarifa za utekelezaji wa majukumu ya serikali katika vyombo vyote vya
habari.Alisema kwa vile viongozi wa chama na serikali hawajibu taarifa
za upotoshaji zinazotolewa na wapinzani, wananchi wanapozisikia
zikirudiwa rudiwa bila kukanushwa wanaziamini.
Social Plugin