Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la
TIENA MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata ya
Bara wilayani Mbozi mkoani Mbeya amenusurika kufa baada ya kutumbukia
chooni wakati akifanya mapenzi huku mumewe akiwa maututi chumban
Habari
za uhakika kutoka kijijini hapo zinadai kuwa mwanamke huyo licha ya kuwa
mke wa mtu alikuwa anafanya ngono chooni na WASI MGALA wakati mumewe
akiwa ndani anaumwa na kwamba alidumbukia choo baada ya banzi alilokuwa
amekanyaga kukatika wakati wanafanya tendo hilo.
Mwanamke
huyo alidumbikia kwenye choo chenye urefu wa futi 17 na kwamba baada ya
kudumbukia, mwanaume aliyekuwa naye chooni wakifanya ngono alikimbia na
kumwacha mwanamke huyo akipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi
walifika na kufanikiwa kumtoa ndani ya shimo na kukimbiza kwenye duka la
madawa linalomilikiwa na muuguzi LEONARD NZOWA ambaye alitoa huduma ya
kwanza kabla ya kumfikisha katika hospitali ya Mbozi Mission.
Hata
hivyo mume wa mwanamke huyo SAIKI GODFREY KAROTI amesema kitendo
kilichofanywa na mkewe ni cha udhalilishaji na si cha uungwana.
source : http://chimbukoletu.blogspot.com/
Social Plugin