Watu wane wameuwa katika nyakati totafuti mkoani Shinyanga,watatu
kati yao kwa kukatwa na mapanga na mmoja kushambuliwa kwa mawe na fimbo na
wananchi wenye hasira kali .
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla
amesema Novemba 27 majira ya saa 3 usiku mwanamke mmoja aitwaye Mhoja Mathias (47)
mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye katika wilaya ya Shinynga vijijini
akiwa amelala na mme wake Mtugwa Mayanga (78) aliuawa kwa kukatwa mapanga
kichwani,kisogoni na mabegani na watu wasiojulikana,na kusababisha kifo chake
papo hapo, huku mme wake akiwa ametolewa nje mbali na nyumba yake na kisha kumtelekeza huko.
Amesema siku hiyo hiyo na muda kama huo, huko katika kijiji
cha Mwasegaki kata ya Solwa tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini
mwanamme mmoja aitwaye Hoja Lusheshanija(35) na mke wake Christina Stephano(29)
wakiwa nyumbani kwao waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga sehemu za shingoni na
mikononi na watu wasiofahamika.
Tayari jeshi la polisi linawashikilia watu watatu watiliwa
mashaka, kuhusiana na tukio hilo,ambao
na Shija Magutabeli,Nkwabi Isheshameja na Marco Manyandodi.
Aidha ameongeza kuwa
huko katika kitongoji cha Igomelo,kata ya Mhongolo wilayani Kahama
mwanamme asiyejulianana jina wala makazi yake ,umri 25-30 alishambuliwa kwa
mawe na fimbo na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kusababisha kifo
chake papo hapo, jana majira ya saa moja
asubuhi.
Kamanda huyo wa polisi amesema vyanzo vya mauaji yote
havijulikani,ambapo uchunguzi bado unaendelea na juhudi za kuwatafuta wahusika
zinaendelea
Social Plugin