WATU wasiofahamika wamevunja Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa Jimbo la Iringa leo usiku, na kumjeruhi vibaya mlinzi wa Kanisa hilo Bw. Bathlomeo Nzigilwa.
Akitoa
maelezo juu ya tukio hilo mhuduma wa Kanisa la jimbo kuu Kihesa, Sista Lucy
Mgata amesema aligundua uvamizi huo alfajiri baada ya kufika kanisani
hapo kwa ajili ya ibada ya Misa za kila siku.
Majambazi
hao wamevunja pia ofisi ya parokia na kuharibu vitabu na kumbukumbu mbalimbali
zikiwa zimechanwa, huku Mavazi ya ibada na vifaa mbalimbali kama misalaba
ikiwa imevunjwa.
Aidha
Sista Mgata amesema watu hao wamechukua fedha za watumishi walizokuwa
wakichangishana, pamoja na hela za chama cha kitume cha utume wa Fatima japo
bado hazijajulikana ni kiasi gani.
Hata
hivyo Padre Aloyce Mdemu ambaye pia ni Makamu wa Askofu wa jimbo hilo, amesema
bado ni mapema kujua thamani ya uharibifu uliofanyika, kwa kuwa wanaendelea na
uchunguzi wa vifaa vingine na maeneo mengine ambayo huenda hawajayabaini.
Muuguzi
mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Iringa Bi. Rustica Tung’ombe amethibitisha
kumpokea majeruhi Batromeo Nzigilwa, na kusema kuwa hali yake ni mbaya na
kuwa anaendelea kupata matibabu.
Source:Blogzamikoa
Social Plugin