JK: AZINDUA TAASISI SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA ARUSHA
Saturday, November 03, 2012
Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara
ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu
cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho,
Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho,
Profesa Burton Mwamila
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha
Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo
cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 02, 2012. Kulia ni
Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo
Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera,
jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt.
DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho,
Profesa Burton Mwamila.
Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na
Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson
Mandera, jijini Arusha.
source:yanayotokeduniani
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin