MAMA MZAZI WA MTOTO ALIYEKATWA MKONO AWASHUKURU WAKAZI WA MBEYA NA MAJIRANI WALIOTOA TAARIFA YA KUTESWA KWA MTOTO WAKE
Sunday, November 18, 2012
MAMA MZAZI WA ANETH ASERA MKANDARA
ANETH SASA ANAEDELEA VIZURI
MAMA ANETH AKIONGEA NA RASHIDI MKWINDA WA GAZETI LA MAJIRA HOSPITALINI HAPO
UMATI WA WAKAZI WA MBEYA WANAOENDA KUMWONA MTOTO ANETH HOSPITALINI HAPO
MAMA wa mtoto Aneth Johanes aliyefanyiwa unyama na hatimaye
kukatwa mkono Asera Mkandara ametoa shukurani kwa wananchi wa Mbeya na majirani
waliosaidia kutoa taarifa na hatimaye kuokoa maisha ya mwanaye aliyekuwa
akiishi kwa mateso.
Bi. Mkandara alizungumza hayo alipotembelewa na wanahabari
waliofika wodi namba 8 kumjulia hali mtoto Aneth na kusema kuwa alipewa taarifa
za kutokea kwa matatizo ya mwanaye lakini hakufafanuliwa ni tatizo gani
alilopata.
Anasema kuwa amewasili Jijini Mbeya akitokea kwao Muleba
Bukoba na kumkuta mwanaye Aneth ambaye ni mtoto wake wa pili baada ya mwanaye
wa kwanza mwenye umri wa miaka 7 anayelelewa na bibi yake mjini Bukoba.
Anasema kuwa hata hivyo yeye hana shughuli maalumu
zinazomuendeshea maisha yake isipokuwa biashara ndogo ndogo hivyo kuchukuliwa
kwa mtoto wake na kaka yake aliyemtambulisha kwa jina moja la Mkandara ilikuwa
ni sehemu ya msaada kwake.
Mama huyo anafafanua kuwa anashukuru kukuta mwanaye ni mzima
na anawashukuru madaktari waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu
zingechelewa angeweza kupata madhara makubwa.
Anasema kuwa kwa sasa anasaidiwa na ndugu na majirani na
baadhi ya watu wanaomiminika hospitalini hapo kutoa msaada.
YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA
NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA MAMA HUYO0756-293784
source:mbeyayetu
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin