Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAUAJI YA KINYAMA IRINGA ,DEREVA BODA BODA AUAWA



Askari  wakitazama Helment ya dereva boda boda iliyokuwa  imeweka juu ya miti
mwili  wa  Dereva boda  boda Abeli Nyunza aliyeuwawa ukiwa  umetupwa katika korongo juu ni dimbwi la damu
Polisi   wakiwa   eneo la  tukio
 Watu  wanaosadikika  kuwa ni vibaka  wamemuua kwa kumpiga  na kitu  kizito  katika paji la uso dereva boda boda eneo la National mjini Iringa Abeli Nyunza na  kumpora  piki piki  yake.

Tukio   hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia  leo katika  eneo la Muungano Frelimo mjini Iringa jirani na  shule ya  msingi Muungano.

Wakielezea   juu ya  tukio  hilo mashuhuda  waliozungumza na mtandao huu  wamedai  kuwa  majira ya usiku  walisikia mlio wa  pikipiki na ghafla ulizimika na baada ya  hapo  ilisikika sauti  ikiita kwa nguvu Peter ! Peter ! mfano  wa  mtu  aliyekuwa  akiomba msaada  na baada ya dakika kama 10 hivi  ukimya ulitanda na ghafla ulisikika  mlio  wa  pikipiki ukiondoka kwa kasi.

Mwenyekiti  wa  boda  boda  mjini Iringa Macurius  Chengulla mbali ya  kuthibitisha  kifo cha  dereva  boda boda mwenzao huyo  bado amesema  kuwa  wameweka  mkakati  wa  kuendesha msako ili  kuwabana  wahusika  wa mauwaji hayo.

Chengulla amesema kuwa matukio  hayo ya  kuuwawa kwa madereva boda boda kwa Manispa ya Iringa ni  tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya  kutekwa na  kujeruhiwa yamekuwa  yakitokea .

Habari na Francis Godwin

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com