Jeneza lenye mwili wa Sharo Milionea likitolewa
Wananchi wakiwa na huzuni wakati mwili wa Sharo Milionea ukitolewa
Umati wa waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Sharo Milionea
Shekh akiombea mwili wa jeneza leye mwili wa Sharo Milionea |
Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Tanga wakiufanyia dua za mwisho mwili wa Sharo Milionea
Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele
Hapa ndipo mwili wa Sharo Milionea ulipohifadhiwa |
Rafiki
mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono
wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.
Mamia ya wakazi wa mkoa wa Tanga pamoja na wasanii wa kundi la Bongo Movie leo wameshiriki kikamilifu katika mazishi ya msanii Sharo Milione yaliyofanyika wilayani Muheza mkoani Tanga umbali wa takribani kilometa 2 kutoka nyumbani kwa msanii huyo huku vurugu za hapa na pale zikitokea wakati wa kuanga mwili huo
Wakati mwili wa msanii Sharo Milionea unaelekea kuzikwa hivi sasa
zimeripotiwa vurugu kubwa kutokea wakati wa mazishi ya msanii
wakati wa shughuli ya kuaga mwili huyo.
Imedaiwa kuwa umati mkubwa wa wananchi wamepata kujitokeza kwa
wingi kuaga mwili wa msanii huyo huku baadhi wakigombea kuaga
mwili huo .
Mwandishi wa mtandao huo ambae anaendelea kuripoti moja kwa moja
(LIVE) kupitia kituo cha radio Nuru Fm pia amesema kuwa kwa
sasa mwili wa Sharo Milionea unatolewa nyumbani kwenda katika
makaburi yaliyoandaliwa
Hata hivyo vurugu hizo zinadaiwa kutokea wakati wa kuaga na kila mmoja akitaka kuugusa mwili wa Sharo Milionea .
Miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliofika ni pamoja na
Nappe Nauye ,Mukama huku Miongoni mwa wasanii waliofika hapo wa
kundi la Bongo Movie ni pamoja na Ray , Kitale na wengine na kuwa
mwili huo umezikwa eneo la umbali wa kilomita 2 kutoka nyumbani
kwa marehemu .
SOURCE:Francisgodwinblog
Social Plugin