Mwanafunzi mmoja aitwaye Danga dwashi (7) aliyekuwa
anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwaningi iliyopo katika Kijiji
cha Mwaningi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ameuawa kwa kukatwa na panga
shingoni na Selemani Lugolola ambaye
alikuwa mchungaji wa ng’ombe hapo nyumbani
kwao.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea wakati
mwanafunzi huyo na mchungaji wa ng’ombe wakiwa wamelala kwenye chumba kimoja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist
Mangalla amesema tukio hilo limetokea Novemba 21 ,2012 majira ya saa nne na
nusu katika kitongoji cha Isambiro,Kijiji cha Mwaningi Kata ya Bulige Tarafa ya
Msalala Wilayani Kahama na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo bado
kinachunguzwa.
Aidha mtuhumiwa wa mauaji Selemani Lugolola alifanikiwa
kutoroka baada ya kufanya mauaji hayo na anaendelea kutafutwa na jeshi la
polisi kwa kushirikana na wadau mbalimbali ili afikishwe katika vyombo vya
sheria.
Kamanda Mangalla ametoa wito kwa wananchi kuwa na tabia
ya kuwafahamu vizuri watu wanaowaajiri ili inapotokea tatizo iwe rahisi
kuwapata.
Social Plugin