Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Butini kata na tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Kashinje Ngasa (60) akiwa amelala ndani ya nyumba yake amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumkata kwa panga na kusababaisha kifo chake papo hapo.
Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo octoba 31 majira ya saa nane usiku ambapo mwanamke huyo akiwa amelala,mme wake aitwaye Kashinje Lugandu (70) alitoka nje kwenda kujisaidia ndipo watu hao walipomkata mwanamke huyo kwa panga na kisha kutoweka.
Social Plugin