Mwanamke mmoja aitwaye Munde Lunyiliga (30) mkazi wa Kitongoji cha Mbapa Kijiji cha Busili Kata ya Bulyanhulu wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mme wake kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea Novemba 26 saa 11 alfajiri mwaka huu,ambapo Mashaka Karuka (40) alimuua mke wake kwa kumpiga fimbo na kisha kukimbia baada ya tukio hilo.
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kamanda wa jeshi hilo ACP Evarist Mangalla amesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa bado zinaendelea.
Social Plugin