Akina mama waombolezaji
wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na
mwanae Ndele Julius(25)
Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele
yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
Kaburi baada ya kuzikwa marehemu
Mkazi wa Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele Julius amemuua mama yake mzazi
kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25
mwaka huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara
baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana mwingine hali
iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani
Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya
mtoto wake na kijana mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo
kuingilia ugomvi huo .
Amesema wakati mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake
alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga
ngumi na mateke mwilini.
Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu
mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka
kupoteza uhai wake.
Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro
Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama
yake marakwamara .
Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata)
umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na
pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi.
Na E .Madafa picha kwa hisani ya Joachim Nyambo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin