Ndani ya kanisa la mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyanga,mahali atakapozikwa Askofu Balina ujenzi wa kaburi ukiendelea leo jioni
Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo la Katoliki la Shinyanga Mhashamu Aloysius Balina aliyefariki dunia Novemba 6, 2102 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza utazikwa kesho katika Kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga saa nne asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya muunganno wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo akiwa ameambatana na baadhi ya mawaziri,lakini pia Rais wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Wilium Mkapa na Mama Maria Nyerere watahudhuria mazishi hayo.Tayari waziri wa ujenzi John Magufuli amewasili mkoani Shinyanga
Jana mwili wa marehemu umepokelewa mkoani Shinyanga ukitokea mkoani Mwanza na kupelekwa katika Kanisa la Moyo Safi wa Maria Parokia ya Shinyanga Mjini,a.mbapo misa takatifu ya kumwombea marehemu ilifanyika ikiongozwa na askofu Renatus Nkwande wa Jimbo Katoliki la Bunda.
Asubuhi ya leo pia kumefanyika misa kama hiyo katika kanisa hilo iliyoongozwa na Askofu Damiani Dalu wa Jimbo Katoliki la Geita lakini pia leo saa tisa alasiri kutakuwa na misa kama hiyo katika kanisa hilo wakati shughuli za kuandaa kaburi atakamozikwa Askofu Balina katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga zikendelea.
Social Plugin