TETESI ZA KUWEPO MISUKULE IRINGA ZASIMAMISHA SHUGHULI ,POLISI WAFIKA KUTAWANYA WANANCHI


 polisi  wakiwasaka  vijana  walioeneza uvumi wa kuwepo kwa msukule eneo la Mwangata mjini Iringa  sasa

 wananchi  wakiwa  wamesitisha  shughuli zao kutaka kuona msukule unaodaiwa kuonekana
 Polisi  wakiwa katika msako wa kuwasaka wazushi wa taarifa  hiyo ya kuonekana mtoto anayedaiwa kufa  siku nyingi a.k.a Msukule
 Polisi  wakiwa katika msako eneo la Mwangata

Zimezuka  habari  zenye utata ambapo inasemekana   kuwa kuna mtoto anayedaiwa kufa na kuzikwa  kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule .

Tukio  hilo  limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa  na kupelekea  polisi  kufika  kuwatawanya  wananchi hao na kuwasaka  wale ambao wanadaiwa kueneza uvumi huo.

Hata  hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya  waliokuwepo hapo ambaye amethibitisha  kuona msukule  huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia .

Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka  kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule  huyo.

Rai ya mtandao  huu kwa jamii ya mkoa  wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuepuka kuamini  imani  za kishirikina ambazo zinaweza kuvuruga amani yetu.

PICHA ZOTE FRANCIS GODWIN

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post