Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ULEVI NOMA: MCHIMBA MADINI AFA BAADA YA KUSUKUMWA KWENYE SHIMO LENYE KINA KIREFU-SHINYANGA

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwabomba,Kata ya Idahina Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga amefariki dunia papo hapo ,baada ya kusukumwa katika shimo lenye kina kirefu katika machimbo madogo ya dhahabu na mchimbaji mdogo wa madini aina ya dhahabu.
Tukio hilo limetokea Novemba 4 majira ya saa nane usiku ambapo walioshudia tukio hilo wamemtaja aliyesukumwa kwenye shimo kuwa ni Mohammed Mathias (28) ambaye pia ni mchimba madini mdogo aina ya dhahabu na alisukumwa na Jackson Shakadi(22).

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo kuwa ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa uliotokana na ulevi wa kupindukia na kuongeza kuwa Jackson Shakadi amekamatwa kwa hatua za kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com