Leo ni siku ngumu kwa mashabiki wa msanii, muigizaji na mchekeshaji
maarufu nchini, Sharo Milionea aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari
alilokuwa akiliendesha kutokea Dar es Salaam kwenda Muheza, Tanga jana
majira ya saa mbili usiku.
Kifo hicho kimewastua wengi lakini zaidi ni kwa Mzee Majuto ambaye
yeye na marehemu walikuwa wametengeneza ‘chemistry’ isiyo na kifani
kutokana na kuigiza filamu pamoja na matangazo ya biashara kama mtu na
mwanae.
Inadaiwa kuwa baada ya kupata taarifa hizo, King Majuto alipandwa na
presha ambapo kwa mujibu wa EATV alikuwa na hali mbaya kutokana na
mshtuko huo.
Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira amesema
marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii
mwenzake John Maganga kuzikwa leo.
Katika hatua nyingine kwenye mitandao ya kijamii kumesambaa ‘screen
shot’ ya meseji ya mwisho aliyokuwa akichat na rafiki yake ambayo
inasomeka Sharo akisema, “Nimekurupuka tu kaka cpo poa kama nimerogwa
hivi. Kuna hela nampelekea mama then narudi tufanye yetu.” Rafiki yake
alimsihi aendeshe kwa umakini kwa kumwambia, “Poa kuwa makini road.”
Nao wasanii mbalimbali pamoja na watu maarufu nchini wamekuwa
wakielezea kwenye mitandao ya kijamii jinsi walivyoshtushwa na kifo
chake:
Adam Mchomvu
danm this jamani daah? Kama ndoto ama story ila ina baki kuwa ukweli
the dude is gone, never came back (sharo milionear)… kapumzike kwa amani
ma men u played ur part so much in ur life time , u made us lough,
happiness, feel good when u do yo thng, amsha amsha type of music yaani
daaah!
Anselm Soggy The-Entertainer
Leo nimezidi kuwa muoga…..KAMA KUNA YOYOTE NIMEWAHI KUMKWAZA NAOMBA ANISAMEHE
Fid Q
Wengi wetu leo baada ya KUAMKA kitu cha kwanza tulichofanya ni
kumshukuru Mungu kwa kuiona SIKU MPYA.. *Naomba tusiusahau huu
utaratibu.
AY
R.I.P Sharo Millionea,Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi,Poleni sana Familia,jamaa na marafiki
Profesa_Jay
Daaah yaani hata bado siamini, naona kama sio kweli hivi ingawa
ukweli ndio huo, Mwenyezi mungu akupumzishe kwa AMANI, Gone too soon
SHALO!!
Vanessa Mdee
Sharo Millionea, Rest in Eternal Peace
DJ CHOKA
Ulivyoanza game watu walikuwa kama hawakuelewi wengine kukucheka na
wengine kukuita mshamba na hata tv walikuwa wanazima..sasa ndio kwanza
mafanikio yalikuwa ndio yanasogea ndugu yangu lakini kazi ya mola haina
makosa kichaa wangu. Nenda mwana kapumzike sasa umetuacha kila mtu
atakupenda na utakuwa star upya na kunawengine watakula kwa mgongo wako
ila baridaa ndio life ya kibongo. RIP
Social Plugin