Watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta chakavu wa nyumba waliokuwa wanauchezea katika Kitongoji cha Galamba Kata ya Kolandoto Wilaya Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 jioni katika kitongoji hicho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amewataja watoto waliofariki dunia kuwa ni Neema Masanja(5) na Emmanuel Masanja (3) na mtoto aliyejeruhiwa kuwa ni juma ngusa (3) ambaye amelazwa katika hospitali ya Kolandoto kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Social Plugin