Mwanamke mmoja aitwaye Asha Damanya (36) mkazi wa kijiji cha Mwamala wilyani Nzega mkoani Tabora amefariki dunia wakati akitoa mimba katika Zahanati ya Matina iliyopo katika kata ya Nyahanga Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema mwanamke huyo alifarika dunia Desemba 19 mwaka huu majira ya saa 12 jioni wakati akitoa mimba katika zahanati hiyo.
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo Kaimu Kamanda wa polisi wa jeshi hilo SSP Onesmo Lyanga amesema tayari wanamshikilia mganga wa zahanati hiyo Damas Matina (63) kwa mahojiano zaidi ,huku akiwaasa wananchi kuacha tabia ya kutoa mimba kwani ni kosa la jinai na ni hatari kwa maisha ya mwanadamu
Social Plugin