Mtoto mmoja aitwaye Malandu Magulumali (3) ameuawa kwa kupigwa fimbo na baba yake mzazi Thomas Paul mkazi wa kijiji cha Kasingilo kata ya ilila wilaya ya shinyanga.
Tukio hilo limetokea Desemba 4 majira ya saa 7 mchana.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema baba mzazi wa mtoto huyo alikuwa anamwadhibu mtoto huyo kwa kumchapa fimbo kichwani siku hiyo,na kufuatia kipigo hicho mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kufariki dunia wakati anapatiwa matibabu.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa kwani alitoroka baada ya tukio hilo.
Social Plugin