Gari
aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama
linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.
Mhudumu
wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja, akiliweka sawa
jeneza baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na
kulisachi. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Watu
wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi,
wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini
hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya shilingi milioni 19.8.
Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.
Jeneza
hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi Munchari Lyoba, mwanafunzi
wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha
SUA.
Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha
hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo Makarang Nouna,
amesema tukio hilo limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na
lilihusisha gari Land Curise lenye namba za usajili SU 37012 na
lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.
Amesema
tukio hilo la kinyamana la kusikitisha, limetokea katika barabara kuu
ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa
jina la Mohammed Trans.
Amesema
walipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa kukatisha
barabara, kitendo kilichosababisha washindwe kupita, na hivyo kutoa
mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la vijana ambao walibeba bunduki mbili
aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
Makaranga
amesema walichofanya kwanza ni kupiga kioo cha gari letu kwa mbele, na
baadaye kumparaza kwa panga usoni dereva wetu Kalistus Malipula.
Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu ambacho tulikuwa nacho.
Akifafanua
zaidi, amesema kwa upande wake yeye ameporwa shilingi milioni mbili
ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi
milioni 8.8 ambazo zilichangwa na wanafunzi kama rambi rambi kwa
mwenzao, na shilingi milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo
zikiwa ni posho.
“Pia tumeporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.
Makaranga
ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika chuo cha SUA,
amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na
kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na
kuruhusiwa.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, ambaye
aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya kutuma
gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa
jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu
waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze
kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Social Plugin